Home Kimataifa Kivumbi cha wikiend hii barani ulaya

Kivumbi cha wikiend hii barani ulaya

8358
0
SHARE

Na Melkizedeck Mbisse

West Bromwich Albion vs Tottenham

Ni mechi ya kukata na shoka, WBA wanaonekana tayari wameshuka daraja kwani wapo nafasi ya 20 wakiwa na alama 28, licha ya kuwa na matokeo mazuri hivi karibuni wakimfunga Manchester United Old Trafford, droo na Liverpool na Newcastle. Ni sawa na wamekumbuka shuka pakiwa pamekucha, Leo Tottenham anaingia uwanjani akijaribu kujihakikishia nafasi ya 4 kwani ana point 70 huku Chelsea ana alama 66 zikiwa bado mechi 3 ligi kufika ukingoni, Tottenham wamekua na matokeo mazuri sana msimu kwa timu ndogo,, wakiishinda Watford jumatatu iliyopita. WBA wana kazi ya kuizua safu ya Spurs chini ya Kane magoli 27 na pasi za magoli 2, Song mwenye magoli 12 na assists 5, Eriksen ana magoli 10 na assists 10, huku Mwiingereza aliyeko katika ubora Dele Ali akiwa na magoli 9 na pasi 10 za magoli,, hivyo nafasi ya ulinzi chini ya Jonny Evans hii leo watakua na kazi ya kuwazuia wachezaji hawa,, licha ya mshambuliaji wa West Bromwich, Rodriguez kuwa katika ubora ila bado hajaweza kufikia hata magoli 10 katika ligi hiyo hivyo ni dhairi kuwa ana kazi ya kufanya dhidi ya ukuta imara wa Spurs chini ya Vertongen, ambapo msimu huu pia Dembele ameonekana kuwa mwiba kwa viungo wa timu pinzani kutokana na mpira wake, na pasi zilizokamilika zaidi pale timu yake inapokuwa inashambulia,, hivyo tutarajie ushindi kwa Tottenham hivi leo..

Everton vs Southampton.

Everton katika uwanja wao wa nyumbani (Goodson Park), katika mechi 6, wameshinda mechi 4 na wapo nafasi ya 8 wakiwa na alama 48, huku Southampton wakionekana kuwa katika hali mbaya msimu huu wapo nafasi ya 18 wakiwa na alama 32, licha ya kushinda magoli 2 dhidi ya Bournemouth kwa magoli ya Tadic, ila leo wana kazi ngumu chini ya kikosi cha Everton ambao wameanza kurejea katika kasi licha ya kuanza vibaya msimu huu,, mshambuliaji mwenye magoli mengi ni Wayne Rooney ambae ana magoli 10 na pasi 2,, ni mchezaji wa kutazamwa katika mechi hii ana uzoefu na ni kiongozi mzuri pale timu inapokua uwanjani,, pia Theo walcot ameleta uhai pale Everton akishirikiana na chipukizi Devies ambae amekua mchezaji wa kutazamwa tokea tulivyomuona pale Taifa zidi ya Gori Mahia, ni mchezaji mwangaikaji, chipukizi na pia mfungaji anapopata nafasi. Naipa nafasi Everton ya kuibuka na ushindi.

RB leipzig vs Wolfsburg.

Baada ya Leipzig kupoteza mechi dhidi ya Mainz magoli 3 kwa 0 weekend iliyopita imewapotezea matumaini ya kuwa katika nafasi nne za juu, wakiwa katika nafasi ya 6 na alama 47, ambapo aliyepo nafasi ya 4 ana alama 52, hivyo bado anataka kushinda ili kujipatia walau nafasi ya kwenda Europa league, Leipzig wana nafasi ya kuibuka na matokeo ambapo katika katika mechi 5 za mwisho wameshinda 4 moja ikiwa dhidi ya Bayern Munich, na wamekua wakiwaonea zaidi Wolfsburg toka wapande daraja, pia Leipzig leo wapo nyumbani ambapo wamekua na matokeo mazuri sana. Wolfsburg ingawa wapo katika kujikwamua kushuka daraja wakiwa na alama 30 katika nafasi ya 16 ila ni dhahiri kuwa mechi ya leo ni ngumu kwao… Wachezaji wa kutazamwa ni Timo Warner, mshambuliaji huyu wa RB Leipzig ana magoli 11 na pasi za magoli 5, huku kwa upande wa Mabingwa wa zamani wa Bundesliga Wolfsburg wana mshambuliaji Daniel Didavi mwenye magoli 8 na pasi 5 za magoli.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here