Home Ligi LA LIGA El Classico: Barcelona wanatuondolea heshima ya soka letu, soka sio Vita

El Classico: Barcelona wanatuondolea heshima ya soka letu, soka sio Vita

9300
0
SHARE
kesho usikose kufika Escape One kucheki mpambano huo na mashindano ya play station

Mimi kama hasimu mkubwa wa barca na nikiwa kama nahodha wa timu nisingeweza kukubaliana hilo lakini kwa kuwa mimi ni mwanamichezo hakuna haja ya kuweka chuki kwenye mafanikio ya mtu mwingine. Inakupasa uheshimu jitihada zao na kuweka roho ya husuda pembeni.

Hayo yalikuwa maneno ya Carlos Puyol miaka 10 iliyopita alipoulizwa kuhusu kuwawekea gwaride la heshima Real Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Mambo yamebadilika. Zidane amesema hiyo heshima haipo. Barcelona waliatawazwa kuwa mabingwa wa la liga baada ya kuwatungua Deportivo la Coruna kwa mabao 4-2. Zidane amesema Barcelona walivunja utamaduni huu baada ya kugoma kuwafanyia katika gwaride la heshima kwenye mchezo wa El classic Desemba mwaka jana walipotwaa kombe la klabu bingwa ya dunia.

wachezaji hawa pekee ndio waliofunga hat trick kwenye Elclassico Jaime LazcanoSantiago BernabéuPaulino AlcántaraLionel Messi na Ferenc Puskás 

Mwandishi: Je utaweka gwaride la heshima pale Camp Nou endapo Barcelona watatwaa ubingwa?

Zidane; Kwanini mnaniuliza hili swali kila siku? Nishasema, hatutafanya hicho kitu, ni maamuzi yangu, wala sitambui hicho mnachosema gwaride la heshima, nishaamua, sitofanya hicho kitu. Wao (Barcelona) waliharibu huu utamaduni.

Zidane kuhsu Mess: Messi anakimbia tu na mpira kuelekea mbele hageuki nyuma. ukimuona anavyocheza unaburudika
No Mchezaji Klabu Magoli
1 Lionel Messi Barcelona 25
2 Alfredo Di Stefano Real Madrid 18
3 Cristiano Ronaldo Real Madrid 17
4 Raul Real Madrid 15
5 Cesar Rodriguez Barcelona 14
5 Francisco Gento Real Madrid 14
5 Ferenc Puskas Real Madrid 14

Assensio; Zidane aliniambia ukiacha Messi hajawahi kuona mchezaji anayetumia mguu wake wa kushoto vizuri kama mimiJe wajua?

Camp Now Maana yake ni Uwanja Mpya

Nimeona kauli ya Ernesto Valverde. Binafsi namuona kama mtu wa kwanza ambaye amesababisha yote haya. Yeye amesema ukitazama soka la sasa hasa kati ya Real Madrid na Barcelona ni mchezo wa kihasimu ambao ndani yake una sumu ya chuki. Hivyo kwake ni ngumu kufanya hivyo maana haoni umuhimu wa hilo na hahitaji kufanyiwa.

ohh Mungu wangu nahisi kuchanganyikiwa. hatuwezi kufanya hiyo heshima. kuiheshimu nyingine kwa gwaride ni kushusha heshima yetu; Valverde kocha mkuu wa Barcelona

KIDOKEZO

Utani wa Real Madrid na Barcelona
                                Real Madrid   
Madrid huwaita mashabiki wa Barcelona El Culers yaani waonesha makalio yao. Hii ilitokana mara baada ya kiwanja chao hapo awali (Camp Nou) kuwa majukwaa madogo na kukosa siti za kutosha mashabiki wao walikuwa wanakaa juu ya ukuta wa uwanja wao kisha makalio yao kuonekana kwa wale wapitaji wa nje ya uwanja.
tazama hii picha kwa makini utaona mshabiki wa Barcelona akimnyooshea Ronaldo kidole kama ishara ya tusi.
                                  Barcelona

 

Mashabiki wa Barcelona wao huwatania wachezaji wa Real Madrid kwa jina la meringues ambayo hii inatokana na jezi zao nyeupe ikimaanisha aina fula ya chakula cheupe kinachotengenezwa kwa mayai na sukari

 

kufikia februari mwaka huu Ramos amepokea jumla ya kadi 274

Ernesto Valvere anachuki zake za wazi ambazo anazificha katika kivuli cha ubabe wa El Classico. Inapokuja suala la heshima lazima tuweke uhasama chini. Miguel Cotto alipochafuliwa uso na Manny Pacquiao lakini bado baada yam echo alimfuata na kumkumbatia.

huyu ni Miguel Cotto; jamaa haoni vizuri lakini ametoa dole gumba kukubaliana na uwezo wa Manny Pac

Hao wanapigana na kuna hasira kubwa ndani yake lakini uhasama wao waliweka pembeni. Miguel cotto huyu huyu licha ya kwamba aliona alionewa kwenye pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather lakini bado alimfuata na kumkubatia. Hata Floyd mwenyewe alimfuata na kumpongeza. 

Rios alipochafuliwa usoni na Manny Pac bado hakususia kabisa kumbatio lake. kama ngumi ina vita kubwa kiasi kile lakini huheshimiana Ernesto anamaanisha nini? Sasa Ernesto leo anataka kutumanisha nini kwenye mpira wa miguu? Nani kamwambia soka lina uadui mkubwa hivyo hivyo? mbona kama huyu kocha ameonesha unazi wa kishamba? leo amegundua wazi Zidane hawezi kufanya hivyo anadai kuwa eti tatizo ni ukubwa wa mechi uliochagizwa na uhasama wao.

Hivi umeshawahi kuona rugby ulivyo na nguvu? kuna fujo sana kule Lakini mchezaji nguli wa zamani wa Scotish mwenyewe Dodie Weir aliwaambia goal.com kuwa inapokuja suala la heshima huo ni utamaduni ambao haumchagui mtu kila mtu anapewa. huyu kocha katoka wapi? mimi nilidhani Barcelona kutokufanya vile labda kulikuwa na sababu nyingine ya msingi kumbe shida alikuwa huyu Valverde? chuki mbaya sana.

Kachumbari

Takwimu; Ushindi mkubwa

10 Real Madrid 11–1 Barcelona 19 Jun 1943 Copa del Rey
6 Real Madrid 8–2 Barcelona 3 Feb 1935 La Liga
5 Barcelona 7–2 Real Madrid 24 Sept 1950 La Liga
Barcelona 6–1 Real Madrid 19 May 1957 Copa del Rey
Real Madrid 6–1 Barcelona 18 Sept 1949 La Liga
Barcelona 5–0 Real Madrid 21 April 1935
Barcelona 5–0 Real Madrid 25 March 1945
Real Madrid 5–0 Barcelona 5 Oct 1953
Real Madrid 0–5 Barcelona 17 Feb1974
Barcelona 5–0 Real Madrid 8 Jan 1994
Real Madrid 5–0 Barcelona 7 Jan 1995
Barcelona 5–0 Real Madrid 29 Nov 2010

Zidane ana gubu au Barcelona wana nongwa?

Gwaride la heshima sio tu utamaduni ila ni heshima ambayo hata Barcelona waliwahi kufanya kwa Madrid.

Lakini nimeona Guilermo Amor aliwajibu kuwa hawawezi kumpa mtu heshima mashindano ambayo wao hawajashiriki. kimsingi Amor alikurupuka kwani mwaka 2006 waliwafanyia hivyo Seville wakati hawakushiriki kombe hilo. Gwaride la heshima halipo tu kwa mashindano ya ndani.

Mwaka 2008 Barcelona iliweka gwaride la heshima kwa Real Madrid baada ya kutwaa ubingwa wa la liga. Pia Barcelona waliwafanyia Sevilla gwaride la heshima baada ya kutwa kombe la UEFA mwaka 2006. Je kwanini waligoma kuwafanyia hivyo Real Madrid baada ya kutwaa kombe dunia la vilabu?

Mfungaji bora Lionel Messi (25)
Idadi ya mechi 270
Assisti nyingi Lionel Messi (14)
Mechi nyingi Manuel Sanchis (43)

 

picha yenye Ballon d’Or 10

imeandaliwa na Privaldinho unaweza pia kunifollow (instagram)

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here