Home Kimataifa Usipokuja Escape One Jumapili kuiona El Clasico, baasi utakosa mambo haya muhimu

Usipokuja Escape One Jumapili kuiona El Clasico, baasi utakosa mambo haya muhimu

9396
0
SHARE

Imebaki leo na kesho tu ,itakapofika Jumapili kutakuwa na ile mechi ambayo inatajwa kuwa mechi kubwa zaidi ulimwenguni kati ya Barcelona vs Real Madrid, wapenda soka wote mjini tutakutana Escape One na kuna sababu kadha wa kadha kwanini uje Escape One.

Andres Iniesta. Mimi binafsi nakwenda Escape kumuona Iniesta kichwani nkikumbuka alivyoshiriki mara nyingi kuiua Madrid ikiwemo zile bao 6-2 walizowahi kuwapiga Bernabeu, Iniesta ametangaza kuondoka Barca na natamani sana kuona El Clasico yake ya mwisho.

Messi na Ronaldo. Muda mwingine unaweza kuhisi kwa sasa hawa ni wakubwa kuliko timu zao, binafsi sina ninayemshabikia kati ya hawa lakini naamini mashabiki wa Lionel Messi watakuja Escape One kwa wingi kumshangilia nyota wao huku wale wa Cr7 nao watamwagika kumtetea Mreno.

Tangu 2014/2015 Barca hajawahi shinda El Clasico nyumbani. Pamoja na Barcelona kuwa nyumbani lakini huu ndio uwanja ambao Madrid hutumia kuwakazia Barca katika El Classico, tangu Luis Enrique ajiunge na Barca hadi sasa hawajawahi shinda Nou Camp katika mchezo huu.

Barcelona watamaliza ligi wakiwa un beaten? Hakuna kitu Madrid watafurahia kama kuisimamisha rekodi Barca wanayoifukuzia ya kumaliza ligi wakiwa hawajafungwa, na El Clasico ndio ambao unaweza kuwa mlima pekee ambao Barca wamebakisha ili kumaliza ligi wakiwa hawajapoteza.

Hali ya kisiasa ya Catalunya. Watu wa Catalunya ambalo ndio jimbo wanalotokea Barcelona wanapigania uhuru wao kutoka Hispania, hii inaifanya Barcelona kuwa na upinzani mkubwa na watu wa Hispania haswa wa jiji la Madrid ambako ndio Real wanapotokea na hii inaufanya mchezo huu kuvuta hisia za watazamaji wengi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here