Home Kimataifa Tujikumbushe namna Salah alivyotua na kuondoka Chelsea miaka 4 iliyopita

Tujikumbushe namna Salah alivyotua na kuondoka Chelsea miaka 4 iliyopita

11857
0
SHARE

Chelsea mwaka 2014 walimnunua Mohamed Salah kutoka Fc Basel, wakati Salah anajiunga na Chelsea mengi yalisemwa na ikiaminika huyu alikuwa Lionel Messi mpya, sio tu mashabiki hadi kocha Jose Mourinho aliamini kuhusu Salah.

Lakini hazikuzidi siku 360 kwa Chelsea kuanza kumchoka Salah, lakini hawakutaka kumuacha moja kwa moja kwani bado waliamini anahitaji uzoefu walimpeleka Italia kwa mkopo, baadae Salah alinunuliwa na As Roma kabla ya kurudi EPL kwa dau la £34m.

Maisha yamekwenda na sasa ni miaka minne baadae Mo Salah anakwenda tena Stamford Bridge, safari hii anakwenda akiwa kama mchezaji anayetajwa kuwa bora zaidi duniani kwa sasa, anaenda Stamford akiwa na tuzo ya PFA, FWA, Mchezaji bora wa Liverpool na akiwa kinara wa mabao Liverpool.

Wakati Salah anajiunga na Chelsea kulikuwa na milima na mabonde ndani ya klabu hiyo, japo kocha Jose Mourinho alikiri kwamba Salah alikuwa aina ya mchezaji ambaye alionekana wazi kutaka kufanikiwa kutokana na jinsi alivyokuwa akijituma.

Mourinho alikuwa akijaribu kutengeneza muunganiko wa wachezaji vijana na aliamini Salah atachukua nafasi ya Juan Mata(aliyesajiliwa United kipindi hicho), na ujio wa Salah utaweza kumuweka pamoja na Oscar,Willian, Eden Hazard na André Schürrle.

Mechi 3 tu za mwanzo kwa Chelsea, ushindi dhidi ya Newcastle, sare na West Brom na kipigo toka kwa City zilitosha kwa Mourinho kuanza kuhoji uwezo wa Salah, Mou akamuonya na kumwambia “hapa sio Basel” akimaanisha ni tofauti kucheza Fc Basel na kucheza Chelsea.

Baada ya mchezo na City kuisha, Jose Mourinho alimuacha Salah nje ya uwanja na hata benchi hakumuweka katika mechi 6 zilizofuata za Chelsea, hadi katika mchezo dhidi ya Arsenal ambao Chelsea waliibamiza Gunners mabao 6-0 huku Salah akifunga bao la kwanza la Chelsea katika mchezo huo.

Baada ya mechi na Arsenal kocha Jose Mourinho aliamini bao lile lilimpa Salah kujiamini, wakati Chelsea inawakaribisha Stoke City katika dimba la Stamford Bridge na kuibuka kidedea cha mabao 3-0 April 5, Mo Salah alikuwa Man Of The Match na Mourinho tena akasema Salah ulikuwa usajili sahihi na anaiweza nafasi ya Mata.

Wakati msimu wa EPL ukiisha, Salah alikuwepo katika kikosi cha Salah kilichokuwa kikijiandaa na msimu mpya na huko ndiko ambako Mourinho alianza kuonesha dalili za kutokumhitaji na hii inatajwa kama sababu ya Salah kuanza kukosa kujiamini na kiwango chake kushuka.

Baada ya mechi za pre-season Salah akaitumikia Chelsea michezo miwili tu na wa mwisho ikiwa ni kipigo toka Bradford katika michuano ya FA, baada ya hapo ndipo safari ya Fiorentina ikaiva na Salah akaenda zake huku Juan Cuadrado akiingia darajani, na huo ukawa mwisho wa Salah kuitumikia Chelsea.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here