Home Kitaifa Shaffih Dauda atoboa siri ya mafanikio Simba

Shaffih Dauda atoboa siri ya mafanikio Simba

13421
0
SHARE

Siku zote mafanikio hayaji yenyewe, yanatafutwa na nyuma ya mafanikio yoyote lazima kuwe kuna mtu au watu wanaopambana kuhakikisha mafanikio hayo yanapatikana.

Kwa sasa klabu ya Simba inaelekea kutwaa ubingwa wa VPL walioupoteza kwa kipindi kirefu lakini pia akuna mgongano wala mvutano ndani ya klabu, kila kitu ni shwari.

Shaffih Dauda anaamini hali hiyo inatokana na uongozi mzuri chini ya kaimu Rais wa Simba Bw. Salim Abdalla maarufu kama try again.

Shaffih ameenda mbali zaidi na kusema kuwa, endapo Bw. Salim ataamua kugombea nafasi ya urais ndani ya Simba bila shaka yoyote atamuunga mkono.

“Wapo wanachama wenye uwezo na nia wakasimama kwenye hivi vilabu vitasogea, mfano mzuri ni Simba ya sasa hivi watu hawajui mafanikio ya Simba ya sasa hivi yapo kwa nani.”

“Salim Abdallah ‘try again’ ni mtu ambaye amesimama amenyooka anasimamia misingi, hana janja-janja nina uhakika aina ya watu kama yeye wanaweza wakawa wanapigwa vita sana na baadhi ya wanachama ambao ni oyaoya.”

“Salim akichukua fomu ya kugombe uenyekiti Simba, mimi kama mpenda maendeleo ya michezo nitamuunga mkono.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here