Home Kimataifa Msuva full mzuka

Msuva full mzuka

11945
1
SHARE

Kiungo mshambuliaji wa Tanzania Simon Msuva usiku wa leo Mei 4, 2018 atacheza kwa mara ya kwanza hatua ya makundi ya vilabu bingwa Afrika wakati timu yake Difaa El Jadida itakapocheza dhidi ya MC Alger ya Algeia.

Msuva amesema anaamini timu yake itafuzu kucheza hatua ya robo fainali ya mashindano hayo kutokana na ubora wa wachezaji wanaunda kikosi chao licha ya kuwa kwenye kundi gumu lenye timu zenye uzoefu na mashindano

“Naiamini timu yangu wa asilimia 100 kwa sababu wapo wazoefu ambao wameshacheza haya mashindano.”

“Nafikiri kila mchezaji atakuwa na ndoto zake kwa upande wangu niliomba sana Mungu tufike hatua ya makundi kwa sababu Difaa sio timu yenye uzoefu sana kwenye haya mashindano lakini inawachezaji wazuri.

Msuva amesema kabla mwaka huu haujaisha atakuwa amepata timu nyingine nje ya Morocco.

“Kwa uwezo wa Mungu tutapambana tutafika na mimi kwa uwezo wangu nina ndoto zangu ambapo nahitaji kupata timu nyingine nje ya Morocco kabla mwaka huu haujaisha.”

“Nataka kupiga hatua nyingine mbele zaidi ya hii ili nibadilike kimpira kwa sababu kila mtanzania ananiombea na kuna watu wanaamini ninauwezo wa kucheza nje, kwa upande wangu nafurahi kuona watanzania wananiunga mkono.”

Comments

comments

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here