Home Dauda TV Video-Manara kapewa onyo kali

Video-Manara kapewa onyo kali

10929
0
SHARE

Bodi ya ligi kuu Tanzania bara imempa onyo kali ofisa habari wa Simba Haji Manara kutokana na kitendo chake cha kuingia uwanjani na kushangilia baada ya mhezo wa VPL kati ya Simba na Yanga uliochezwa Aprili 29, 2018.

“Mkuu wa idara ya habari wa klabu ya Simba Haji Manara tumempa onyo kali kwa sababu baada ya mechi ya Simba na Yanga aliingia uwanjani na kushangilia kwa kucheza”-Boniface Wambura, ofisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi.

Kitendo alichokifanya kinakiuka kanuni ya 11 ambayo inasema wazi kabisa watu wasiohusika na eneo la uwanja hawaruhusiwi kuingia eneo la uwanja kabla, wakati na baada ya mechi.

Iwapo vitendo hivyo vitaendelea tutachukua hatua kazi zaidi, kwa hiyo adhabu yake ni tumeitoa kwenye kanuni ya 14 kanuni ndogo ya 49 ya ligi kuu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here