Home Ligi EPL Tusimnafikie Iniesta huku tunamkebehi Salah

Tusimnafikie Iniesta huku tunamkebehi Salah

16905
0
SHARE

Iniesta amemaliza na Barcelona. Yupo sahihi kabisa. Barcelona ipo hivyo. Wana fadhila lakini hawana huruma. Umri ukienda hata kama kiwango chako ni kikubwa lazima uwapishe wadogo zako. Sawa.

Nachojiuliza kwanini watu wanamdanganya Iniesta? Nimewaza sana. Wajuaji tumekaa kitako na kulalamika eti iniesta anaondoka bila Ballon d’Or. Hapana. Mpira haupo hivyo. Hakuna BDO iliyokuwa halali mbele ya Iniesta. Mnaponzwa na hisia bila kujali uhalisia.

Watu kama akina Ramso Mtubabu, Isack Nyenza na Shaban Ramadhani wataniambia 2010 Messi hakustahili. Sawa nani alistahili sasa? Wapo watakaomtaja Sneijder na wenye roho ngumu watamtaja Iniesta. Sasa nawauliza tena kwa mara nyingine ni BDO ipi aliyostahili Iniesta? Au tufanye hii ya 2010 Sneijder hakuwepo tumsimamishe Messi, Iniesta na Xavi.

Watu wengi sio wafuatiliaji. Tunapenda sana kudakia mambo juu kwa juu. Ukweli ni kwamba BDO ni mafanikio ya mchezaji binafsi ndani ya klabu yake na taifa lake haya mengine yaliletwa na Sepp Blatter ili kuwatofautisha Messi na Ronaldo basi. Huyu Iniesta la liga hakuwa tegemezi hata kidogo ndani ya Barcelona kwa mwaka 2010. Alicheza michezo 29, katika majira ya joto alicheza dakika 90 kwenye michezo 7 tu iliyobakia alianzia benchi au alitokea benchi. Aliandamwa sana na majeraha UEFA alicheza michezo 9 na hapo Barcelona ilitolewa na Mabao ya Sneijder, Maicon na Milito.

Iniesta 2010 hakuwa mchezaji bora wa la liga, hakuwa mchezaji bora wa Hispania, hakuwa mchezaji bora wa Kombe la Dunia, hakuwa mchezaji wa bora wa uefa wala copa de ray, sasa mnataka awe mchezaji bora wa dunia hapo kwa kigezo gani? Mo Salah mwaka huu ametwaa tuzo tatu kubwa, ameweka rekodi kadhaa ndani ya uefa, EPL na Afrika. Je siku akiondoka nae mtasema haya mnayosema kwa Iniesta? Kwa Kebehi zao watakwambia Salah bado sana.

Na wana iman atakosa tuzo hii ya dunia kwa sababu hizo hizo za roho ya korosho. Lakini ni wazi ana msimu bora sana kuwazidi hata wale wanaotembelea majina yao na ukubwa wa vilabu vyao.

Ni kweli Iniesta alifunga bao dakika ya 116 kwenye kombe la dunia lakini hilo latosha kumpa BDO? Kwa kipi? Kwanza Ukisema wampe BDO kwa sababu ya kombe la dunia ni kuwakosea adabu na heshima Iker Casilas, Puyol, David Villa aliyekuwa kinara wa mabao (5) kombe la dunia na kiungo bora kabisa Xavi Hernandez.

Orodha ya wachezaji waliofanya vizuri kwa Hispania kombe kombe la dunia ilikuwa ni 1. Iker Casilas 2. David Villa 3. Xavi Hernandez, Iniesta hakuwepo kwenye tatu bora wala 5 bora. Kuna mtu kanifinya hapa kaniambia nyamaza maana 2012 Iniesta alikuwa mchezaji bora wa Euro na Hispania wakatwaa kombe la Euro, kidogo nimzabe vibao. Hivi kweli rekodi ya Messi ya magoli 94 kwenye mechi 79 iniesta hapo angepeleka vipi pua? Huo mwaka tusiujadili kabisa

Kipara ni mchezaji mzuri sawa lakini sio mbele ya Wesley Sneijder aliyekuwa kinara wa Mabao kombe la Dunia (5), aliyefunga mabao muhimu kuanzia hatua ya makundi ya UEFA hadi nusu fainali kisha kutengeneza bao la kwanza la Diego Milito kwenye fainali pale pale Bernabeu ambapo walimdharau. Sneijder alikuwa na msimu mzuri hasa pale alipojenga himaya yake na kuthaminika kama kiungo mshambuliaji bora na wa hatari zaidi kwa mwaka ule.

Umuhimu wa goli la kombe la dunia wa Iniesta hautoshi tu kumpa kibuyu cha dhahabu. Kama ni magoli muhimu bila Shaka Diego Millito alipaswa kuwa mchezaji namba 2,3 au hata 1 kwa kigezo hicho. Unataka na Gotze nae tuseme alikuwa muhimu? Kama kombe la dunia lingekuwa na umuhimu huo basi Diego Forlan mchezaji bora wa kombe la Dunia angetwaa tuzo hiyo.

Kuna watu wana gubu sana, yaani mwaka huu roho zinawauma sana. Yaani ukimuuliza kuhusu BDO watakimbilia kombe la Dunia. Watakwambia hilo ndio litakalo amua mchezaji bora. Mbona Messi 2014 pamoja na Neuer walifanya vizuri kombe la dunia lakini tuzo ikaenda kwa Cristiano?

Kati ya vipindi ambavyo BDO ilitolewa kwa kuzingatia zaidi hasa malengo na matakwa ya nini maana ya tuzo ya mchezaji bora wa dunia basi ni 2010 (Messi) 2012 (Ronaldo) na 1999 (Rivaldo) pamoja na ile ya Romario 1994. Kinachoangaliwa zaidi ni ubora wa mtu na sio mafanikio ya timu. Kwa mfano messi 2010 timu yake ya taifa ilikuwa na kocha mbovu (Maradona) huwezi kumlaumu hata kidogo, mwaka huo huo alifunga magoli 42 michezo 36 ya ligi na asisti 13. Sasa kweli kwa takwimu hizo tuamini Iniesta alistahili? Messi alikuwa mchezaji bora wa la liga (Salah Mchezaji bora wa EPL), Messi akawa mshambuliaji bora wa la liga ( Salah mchezaji bora Africa).

Messi hakuwa na tuzo nyingine, Salah amebeba tuzo ya waandishi wa habari na kuweka rekodi ya mchezaji bora wa Mwezi mara tatu mfululizo na Uefa pia.

Mtu pekee wa kulia ni Sneijder lakini kwa bahati mbaya alikutana na mchezaji aliyekuwa na kipaji cha pekee na aliyefanya makubwa pia. Sneijder alitwaa makombe matatu lakini bado Messi alipagawisha wapiga kura hasa kwa umri wake (23) na uwezo alionesha.

Msimu huu Salah ana mafanikio binafsi zaidi kumzidi iniesta wa 2010. Wapo wanaosema Salah bado ni mchanga. Tatizo wanapenda kuandika lakini hawajui kusoma. Salah amewahi kuwa mchezaji bora wa ligi ya Uswis, mfungaji bora wa As Roma 2015, mtengenezaji magoli mengi As Roma 2016, Mfungaji bora Kufuzu kombe la dunia 2014 (6) na 2018 (5). Mnataka afunge magoli yanayovunja magoli au?

Niwambieni tu hakuna Tuzo Iniesta aliwahi kustahili mbele ya Messi na Ronaldo. Kuhusu Sneijder tunaweza kuongea ila tunamponza kipara huku tuna mkebehi Salah. Mnaboa

Imeandaliwa na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here