Home Kitaifa “Nchi hii haimuoni Mkude? Au kwakuwa hachani nywele?” Haji Manara

“Nchi hii haimuoni Mkude? Au kwakuwa hachani nywele?” Haji Manara

12448
0
SHARE

Ofisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara kupitia ukurasa wake wa instgram ame-post ujumbe amihoji maswali kadhaa kuhusu Jonas Mkude kuchukuliwa poa Tanzania.

Manara amehoji kwamba nchi hii haimuoni Jonasi Mkude? Tatizo ni jina lake la Kiluguru au kwa kuwa hachani nywele? Halafu mwisho amesema kwa sasa hakuna mbadala wake nchini.

Ujumbe huo ame-post Jumatano Mei 2, 2018 unasomeka hivi:

“Leo nimekaa nikajiuliza swali moja gumu kisha nikakosa majibu…hivi nchi hii haimuoni Jonas Mkude? Tatizo ni nini au hilo jina lake Mkude limekaa Kiluguru sana au kwa kuwa hachani nywele? Huyu jamaa  amezaliwa midfielder na kwa sasa akuna mbadala wake kwenye nchi hii ya JPM.”

“Please jamani tuwe serious na vipawa vya watu.”

Manara aliwahi kuhoji pia kuachwa kwa Mkude kwenye kikosi cha timu ya taifa kilichotajwa kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki za kalenda ya Fifa dhidi ya Algeria na DR Congo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here