Home Dauda TV Video-Mate yamponza Yondani

Video-Mate yamponza Yondani

13699
0
SHARE

Bodi ya ligi kuu Tanzania bara imemsimamisha beki wa Yanga Kelvin Yondani kutokana na kumtemea mate Asante Kwasi katika mhezo wa VPL kati ya Simba na Yanga uliochezwa Aprili 29, 2018.

Yondani amesimamishwa hadi hapo suala lake litakapotolewa maamuzi na kamati ya nidhamu ya TFF.

“Kelvin Yondani tumemsimamisha mpaka suala lake la kumtemea mate Asante Kwasi litakaposikilizwa na kamati ya nidhamu ya TFF na kutolewa uamumuzi”-Boniface Wambura, mtendaji mkuu bodi ya ligi.

“Hili ni suala la kinidhamu na sisi tumelichukua na kulipeleka kamati ya nidhamu kwa ajili ya hatua za kikanuni zinazoendesha ligi pamoja na kanuni za nidhamu za TFF.”

“Uamuzi wa kumsimamisha umefanywa kwa mujibu wa kanuni ya tisa kanuni ndogo ya tano ya ligi kuu ambayo inatupa fursa ya kumsimamisha mtu anapokuwa anakwenda kwenyd vyombo vya haki vya TFF .”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here