Home Kimataifa LeBron James anatajirika tu namna Liverpool wanavyong’ara

LeBron James anatajirika tu namna Liverpool wanavyong’ara

12545
0
SHARE

Mwaka 2011 mchezaji wa Cleveland Cavaliers LeBron James aliwekeza kiasi cha hisa zenye thamani ya £4.8m katika klabu ya Liverpool ikiwa ni 2% katika uwekezaji wa klabu hiyo yenye makazi yake Anfield.

Wakati LeBron anawekeza Liverpool wengi walimnyooshea kidole na kudai kwamba amgeweza kufanya uwekezaji mkubwa zaidi na ambao ungempa faida kubwa zaidi kuliko huu aliofanya kwa Liverpool.

Miaka imekwenda na sasa thamani ya hisa alizowekeza LeBron zinatajwa kupanda kutoka £4.8m aliyowekeza mwaka 2011 hadi kufikia kiasi cha £25m, hii ikimaanisha ameongeza faida zaidi ya £20m.

LeBron alifanikiwa kupata sehemu ya umiliki wa klabu ya Liverpool baada ya kampuni yake ya michezo kuingia mkataba wa ushirikiano na kampuni ya Fenway Sports Partners ambayo inaendeshwa na moja ya wamiliki wakuu wa Liverpool Tom Werner na John Henry.

Mwaka jana jarida la Forbes lilimtaja James kama mwanamichezo namba mbili anayelipwa zaidi baada ya Cristiano Ronaldo, huku mwaka jana pekee akiwa ameingiza kiasi cha £63.4 katika mfuko wake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here