Home Kitaifa Kabwili aiacha Ngorongoro Heroes

Kabwili aiacha Ngorongoro Heroes

12035
0
SHARE

Wakati timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ ikijiandaa kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Mali kuwania kufuzu fainali za Afrika, golikipa namba moja wa timu hiyo Ramadhani Kabwili hatokuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza mchezo wa kwanza Dar.

Kocha wa Ngorongoro Heroes Ammy Ninje amesema Kabwili atakuwa na majukumu kwenye klabu yake ya Yanga hivyo watafanya maboresho katika eneo hilo.

“Tutafanya maboresho kwenye eneo la golikipa kwa sababu Kabwili hatokuwa na sisi atakuwa kwenye majukumu na Yanga, tuna golikipa mmoja tutamleta mwingine kutoka Zanzibar kwa hiyo ni eneo hilo tu ndio litafanyiwa maboresho.”

“Golikipa kutoka Zanzibar namfahamu kwa jina moja tu Seif anatoka JKU, akija tutam-assess atajiunga na sisi.”

“DR Congo ilikuwa timu ngumu lakini tulifanikiwa kuwatoa, tunaheshimu timu zote ambazo zipo kwenye mashindano lakini kitu muhimu ni matayarisho. Tukifanya matayarisho na wachezaji wangu wakachukua misingi tuliyopeana basi mechi inaweza kuwa rahisi.”

“Kwenye timu yoyote hayawezi kukosekana makosa ndiyo maana tunafanya marekebisho. Wachezaji wanajituma vizuri uwanjani wanafuata maelekezo tunayowapa na unaona kila mchezaji ana hamu ya kuanza.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here