Home Kimataifa Utabiri wa Geoff Lea na Charles Abel na kilichotokea Real Madrid vs...

Utabiri wa Geoff Lea na Charles Abel na kilichotokea Real Madrid vs Bayern Munich

10604
0
SHARE

Real Madrid imeandika rekodi ya kufuzu fainali ya UEFA Champions League kwa mara ya tatu mfululizo baada ya sare ya 2-2 dhidi ya Bayern Munich kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu hivyo Madrid kusonga mbele kutokana na ushindi wa 2-1 waliopata ugenini katika mchezo wa kwanza.

Kabla ya game hiyo wadau mbalimbali walikuwa na maoni tofauti kuhusu pambano la nusu fainali ya pili kati ya Madrid na Bayern Munchen.

Kupitia Sports Xtra ya Clouds FM walisikika Geoff Lea na Charles Abel walitoa maoni yao kabla ya game hiyo iliyokuwa ikiamua timu itakayokuwa ya kwanza kufuzu fainali ya UEFA Champions League msimu huu.

Geoff Lea

Mechi ya Real Madrid na Bayern Munich bado ni mbichi sana kwa ninavyoitazama lakini watu wanaweza kushawishika kwamba Madrid ana mguu mmoja kwenye fainali kutokana na ushindi wa 2-1 alioupata ugenini kwenye mechi ya kwanza.

Naamini kwamba Bayern Munich ni timu kubwa yenye vigezo sawa na Madrid kwa hiyo wana nafasi ya kupata matokeo kwenye mchezo wa ugenini kama ilivyokuwa katika mechi ya Madrid na Juventus hatua iliyopita.

Bayern wanakabiliwa na changamoto moja wanapokuwa wanacheza nje ya Ujerumani hasa siku za hivi karibuni ambapo wamekuwa wakitawala sana ligi ya Ujerumani. Mara nyingi hawapati changamoto kama timu za Madrid, Atletico Madrid, Barcelona, Man City, Liverpool wamekuwa wakizipata kutokana na ushindani wa ligi zao ambazo zinazikomaza timu hizi na hii ndio hasara ambayo Bayern imekuwa ikipata.

Ni mara chache unaweza kuona udhaifu wa kiufundi wa Bayern ikiwa kwenye ligi yao, jambo hili linaweza kuwanyima fursa ya kuingua fainali kama watacheza bila kuwa na uangalifu wanaopaswa kuwanao kutokana na mazoea ya kucheza kwenye ligi ambayo kwa kiasi kikubwa ni ligi dhaifu.

Vinginevyo kurejea kwa wachezaji muhimu kitakuwa kitu muhimu sana kwa Bayern kwa sababu pamoja na uongozi wa Madrid walionao, tunafahamu udhaifu wa safu ya ulinzi ambao ulitumika kufungwa magoli manne ya mwisho kwenye upande wa Marcelo akipanda kushambulia na kusahau majukumu yake kama mlinzi.

Hayo mambo yote yanaweza kuwa faida kwa Bayern na udhaifu kwa Madrid ambao hawajaweza kuupatia ufumbuzi, naamini Madrid wanaweza hata kutolewaa kwenye hatua hii. Siwezi kusema mechi imeisha kwa sababu ya matokeo waliyoyapata kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Alianz Arena.

Charles Abel

Ni mchezo mgumu kwa sababu matokeo ya kwanza hayajawa na taswira ya moja kwa moja kwamba Madrid imefuzu fainali kwa sababu matokeo ya 2-1 maana yake Bayern inahitaji kupata angalau kuifunga Madrid 2-0 uwanja wa Bernabeu kitu ambacho Ulaya kinawezekana.

Naona Madrid wana nafasi kubwa ya kupata ushindi dhidi ya Bayern kwa sababu ni timu inayocheza kwa mahesabu zaidi na sio ufundi, ukirejea mchezo wa kwanza Bayern walimiliki mpira kwa muda mrefu mwisho wa siku Madrid wakapata matokeo.

Kikubwa kinachonifanya niwape nafasi Madrid, Bayern Munich ni timu inayokosa ubunifu katika eneo la mwisho la timu pinzani tofauti na Madrid ambao wanaweza kukaa nyuma na kumudu mashambulizi ya kushtukiza, ni mchezo mgumu lakini nawapa nafasi Madrid ya kupata matokeo na kufuzu fainali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here