Home Kitaifa Ukurasa wa Adam Salamba: wazungu sio wanafiki

Ukurasa wa Adam Salamba: wazungu sio wanafiki

16417
0
SHARE

Mwaka 1997 kule kakola Shinyanga ndiko alikozaliwa bwana Salamba. Alibatika kupata elimu ya shule ya msingi katika shule Kakola kabla ya kwenda shule ya sekondari Bulyanhulu na kupata elimu hadi kidato cha 4. Akiwa na umri mdogo kiwango chake kilionekana kuwa maradufu na alijizolea umaarufu mkubwa katika Shule alizosoma.

Maisha yake 2015.
Alianzia maisha yake katika klabu ya Bulyanhulu ambayo ilikuwa daraja la tatu. Jitihada zake ndizo zilizoiwezesha klabu hii kwa mara ya kwanza kuvuka daraja la tatu na kwenda daraja la Pili.

Ajiunga na Polisi ya Zanzibar
Mwaka 2016 alipata nafasi ya kwenda kucheza katika klabu ya Polisi Zanzibar. “Nilikuwa najituma sana mazoezini, na kiwango changu kiliwashawishi sana Ma bosi klabu hiyo”

Alipokwenda Zanzibar aliichezea klabu hiyo kwa miezi minne tu. Baadhi ya mambo hayakwenda sawa. Mwisho niliamua kurudi Nyumbani”– Salamba

Akutana na shaffih dauda, atwaa tuzo

Katika kumbukumbu ya maisha yangu siwezi kusahau mashindano ya Brazuka. Nakumbuka nilikuwa mchezaji bora wa mashindano hayo na ilikuwa mara yangu ya kwanza kuonana na Shaffih Dauda.

Nilifarijika sana kumuona na alinihoji kisha akanipa mausia. Katika michuano ile mshindi wa kwanza alikuwa anabeba milioni 4 na wa pili milioni 2. Mashindano yale yalinitia sana hamasa ya kutaka kuendelea kufanikiwa zaidi” alisema Salamba.

Huenda nawe ni kijana mdogo upo mtaani na umeshirikii mara kadhaa mashindano mbalimbali. Usidharau nafasi uanyopata pata hata kama ni kombe la mbuzi ila uongeze bidii ufike alipofika Mbwana Samatta. Shida kubwa aliyokumbana nayo katika maisha yako ya soka ni kukosa msaada wa kufikia malengo yake. “naweza kusema kwangu mimi sikupata sapoti kubwa sana, maana asilimia kubwa ya majukumu yangu yote ya kisoka nilijitegemea kwa kiasi kikubwa” salamba.

Hili linaweza kuwa tatizo kwa baadhi ya vijana wadogo wanotaka kufanikiwa katika soka. Wengi wao wanahitaji kushikwa sana mkono ili wafike mbali. Sawa wapo wengi ambao kwa namna moja au nyingine wamesaidiwa lakini sio lazima. Salamba leo yupo Lipuli na hakuwahi kubweteka au kulalama kukosa msaada. na bado anapaswa kutia bidii kufika mbali zaidi.

Afanya majaribio Stand United
Baada ya mizunguko mingi mwaka 2016 alipata nafasi ya kwenda kufanya majaribio katika klabu ya Stand United. Siku ya kwanza kufika mazoezini alikuta na kocha Mzungu Patrick liewig.

Siku ya kwanza tu ya mazoezi kocha aliridhika na kiwango cha Salamba. Siku ya pili alifika mazoezini asubuhi na Mapema akiwa na baiskeli ya Marehemu mzee salamba mwalimu liewig akamwambia kuanzia leo utakuwa unafanya mazoezi kama mchezaji wa kikosi cha timu ya kwanza. Wazungu sio wanafiki

Maisha ya Stand yalikuwa magumu sana. Ilikuwa ndio msimu wao wa kwanza kupanda ligi kuu hivyo baadhi ya mambo hayakwenda sawa. Ukata ulisababisha klabu hiyo ishindwe kufanya vyema na kusuasua.

Apata nafasi kucheza Ligi kuu
Mwenyekiti wa Stand United Dr Ellyson Maeja ndiye aliyewatambulisha Salamba na wenzake mnamo mwaka 2016 mwezi wa sita ikiwa ni maandalizi ya ligi kuu. Mchezo wake wa kwanza ligi kuu ilikuwa dhidi ya Azam tarehe 12-10-2016 siku ya jumatano katika uwanja wa Kambarage. Alitokea benchi dakika ya 16 baada ya Chidiebere kuumia na alifunga goli ambalo liliamua matokeo mpaka mwisho

Katika michezo 13 Aliifungia Stand United magoli manne pekee. Licha ya kwamba nafasi ya kudumu katika kikoi cha kwanza lakini bado hakukata tamaa. Sekeseke la mishahara lilikwamisha juhudi zake za kuendelea kuipigania Stand United. Baadae aliuomba uongozi wa Stand umruhusu aondoke.

nilikuwa nawadai hela nyingi sana, mara kadhaa nilicheza bila kulipwa. Mimi nina wadogo zangu wawili wote wanasoma na wananitegemea mimi kama kaka je nitawasaidia vipi”? alisema Salamba.

Baada ya muda mrefu wa mvutano aliwaomba wamruhusu aondoke na aliwaahidi kuwa wakimuacha akiendelea na maisha yake mengine hatowadai hela alizokuwa anawadai.

Baadhi ya Wachezaji waliosajiliwa na Stand mwaka ule Jina Klabu atokayo
Erick Muriro Toto Sports Club
Miraji Musa Maka Toto Sports Club
Adam Salamba Bulyanhulu
Charles Ibreck Bulyanhulu
John Biseko Bulyanhulu

Atimkia LIpuli.
Siwezi kumsahau kocha Hemed Morocco alinisaidia sana baada ya kuchukua nafasi ya Kocha wa awali ya Bw. Patrick Liewig. Alinipa nafasi kubwa ndipo nikaonesha uwezo uliowavutia sana Lipuli” Salamba.

Maisha ya Lipuli yalikuwa ya tofauti sana kwake hasa hasa hali ya hewa ya Iringa. Alipata tabu sana na mara kadhaa alikuwa akiugua kifua. Tokea aliposajiliwa katika kipindi aliposajiliwa katika dirisha dogo mwaka 2018 alifunga magoli matano kwenye michezo 8 ya awali.

Timu ya taifa
Nina ndoto za kucheza timu ya taifa, natamani siku moja nami nivae uzi huo kuonesha namna navyoweza kuipambania Stars.

Nilipofanya vizuri michuano ile ya ACACIA niliitwa na Mwalimu Salumu Mayanga na Mart Noij kwenye kikosi cha Maboresho. Kwa sasa yupo timu ya U-23

Maisha binafsi

Siku moja baada ya mechi nilirudi nyumbani. Baadae nikatoka na marafiki zangu kwenda kijiweni kupiga stori. Nilipofika tu pale kijiweni nikapigiwa simu mama amefariki. Nilihuzunika sana. Baada ya mwezi mmoja baba nae akafariki-Salamba.

Alizaliwa tarehe 25-11-1997 kule Kakola Shinyanga. Ni mtoto wa pili katika Familia ya mzee Salamba. Ana Dada yake mkubwa, na wadogo zake wawili, wa kiume na wa kike. Yeye ni mshambuliaji wa kati yaani namba 9. Yeye ni mshabiki wa Arsenal na anampenda Sana Cristiano Ronaldo.

Kwa Tanzania anamkubali John Bocco kwani anacheza namba sawa na yeye na anapenda anavyojituma. “messi anajua sana mpira lakini nampenda sana Ronaldo hasa anajituma sana”. Mwezi machi mwaka 2018 alitwaa tuzo ya mchezaji bora baada ya kufunga magoli 3 kwenye dakika 269 baada ya kuwapiga chini Salum Kimenya wa Prison na mlinda mlango wa Azam. Alitwaa tuzo hiyo baada ya kushinda michezo miwili na kutoa sare mmoja na klabu hiyo kupanda hadi nafasi ya 7.

Imeandaliwa na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here