Home Kimataifa Liverpool kuifuata Real Madrid au Roma kuishangaza dunia hii leo?

Liverpool kuifuata Real Madrid au Roma kuishangaza dunia hii leo?

9839
0
SHARE

Tayari Real Madrid wametangulia fainali za Champions League msimu huu, Liverpool leo wanakuwa wageni wa As Roma huku Liverpool ikiendelea kubaki kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mechi hata moja katika Champions League msimu huu.

Pamoja na maajabu ambayo As Roma waliyafanya mbele ya Barcelona, lakini historia hii leo inawabana kutokana na kwamba rekodi inaonesha hakuna timu ambayo imewahi kupindua matokeo ya bao 5-2 baada ya kipigo cha mechi ya kwanza.

Liverpool sio wageni wa nusu fainali hata kidogo, hii ni nusu fainali yao ya 10 ya michuano hiyo. Katika nusu fainali 9 zilizopita walikwenda fainali mara 7, ni Ac Milan tu na Chelsea ndio ambao walifanikiwa kuisimamisha Liverpool katika nusu fainali.

As Roma hawajawahi kuwafunga Liverpool katika michiano ya Ulaya, wameshacheza mara 4 na Liverpool akishinda 2 na suluhu 2, moja kati ya suluhu hizo ni fainali mwaka 1984 ambapo Liverpool walishinda mchezo huo kwa penati 4-2.

Uwanja wa nyumbani wa As Roma inaonekana kama mahala pao pa kujidai sana kwani hadi sasa hawajaruhusu wavu wao kuguswa katika uwanja wao katika mechi zao zote 4 zilizopita za CL nyumbani kwao, ila hawajawahi kushinda mechi 5 mfululizo za CL.

Tangu mfumo mpya wa Champions League utangazwe mwaka 2003/2004 Real Madrid wamefunga mabao 41(2013/2014) katika michuano hiyo na ndio timu pekee iliyofunga mabao mengi kuliko Liverpool (38) katika michuano hiyo, huku Liva wakiwa timu inayoongoza kwa mabao mengi katika msimu mmoja katika CL kutoka EPL.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here