Home Kimataifa Liverpool haooo wanakwenda Kiev

Liverpool haooo wanakwenda Kiev

11186
0
SHARE

Pamoja na kipigo cha mabao 4-2 kutoka kwa As Roma, lakini Liverpool wamefanikiwa kufudhu kwenda fainali ya michuano ya Champions League kwa aggregate ya mabao 6-7, na hii ikiwa ni fainali yao ya 8 wanakwenda.

Roberto Firminho alitoa assist iliyozaa bao la kwanza la Liverpool lililofungwa na Sadio Mane, assist ya Firminho inamfanya kuwa mchezaji wa kwanza katika miaka 10 ya mwisho ya CL kuwahi kuwa na walau mabao 7 na assist 7 katika msimu mmoja wa CL.

Dakika ya 15 ya mchezo, As Roma walipata bao baada ya James Milner kujifunga. Hili linakuwa bao la kwanza kwa Liverpool kujifunga tangu Johne Arne Riise ajifunge katika mchezo wa nusu fainali vs Chelsea msimu wa 2007/2008.

Dakika ya 25 Liverpool walipata tena bao la kuongoza kupitia kwa Gerginio Wijnaldum, na hili likiwa bao la 19 kwa Wijnaldum kuwahi kuzifungia timu za Uingereza, 11 akiwafungia Newcastle na 8 akiwafungia Liverpool.

Bao la Mane limeufanya utatu wa Liverpool kufikisha jumla ya mabao 29 katika Champions League msimu huu, sasa Mane, Salah na Firmino wanakuwa wamefunga mabao mengi kuliko Bale, Benzema na Cr7 walivyofunga msimu wa 2013/2014 (28).

Bao la leo la Edin Dzeko linamfanya kufunga mabao 5 katika mechi 5 mfululizo za CL na sasa anakuwa mchezaji wa kwanza wa As Roma kuwahi kufunga mabao 5 katika michezo 5 mfululizo ya klabu hiyo katika Champions League.

Lakini pia bao la Edin Dzeko linamfanya kuifikia rekodi ya Samuel Etoo ya mchezaji wa klabu toka Italia kuwahi kufunga mabao 8 katika Champions League, rekodi aliyoweka mwaka 2010/2011, Radja Nainggolan alifunga mabao mengine mawili kwa As Roma.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here