Home Kimataifa As Roma wavaa jezi ya Sean Cox kuelekea mchezo wao zidi ya...

As Roma wavaa jezi ya Sean Cox kuelekea mchezo wao zidi ya Liverpool

10317
0
SHARE

Katika kuonesha kwamba soka ni mchezo wa kiungwana, wachezaji wa As Roma wote wameonekana kuvaa jezi zenye jina la Sean Cox wakati wakijiandaa kuelekea pambano lao la nusu fainali dhidi ya Liverpool.

Sean Cox 53 ni mshabiki wa Liverpool ambaye siku chache zilizopita alipigwa na mashabiki wa As Roma hadi kupoteza fahamu wakati wa pambano la kwanza la nusu fainali kati ya Liverpool na As Roma.

Jana wakati wa mazoezi ya Roma jezi zao zilikuwa zimeandikwa “Forza Sean” hii ikiwa sehemu ya mashabiki hao kumtakia kila la kheri Sean ambaye bado yuko hospitali akiendelea kupigania uhai wake.

Taarifa zinadai hali ya mshabiki huyo bado haijatengemaa, As Roma imewataka mashabiki wao kuepuka vitendo vya namna hivyo ambavyo vinaonekana kuichafua image ya klabu hiyo.

Naye kocha wa Liverpool amezungumzia kitendo cha As Roma kuvaa jezi za kumtakia kila la kheri Sean kama kitendo cha kiungwana katika soka, na kusisitiza kwamba soka ni uungwana na mashabiki wote pamoja na tofauti zao uwanjani ila ni kitu kimoja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here