Home VPL Asante Kwasi, Asante sana Yondani

Asante Kwasi, Asante sana Yondani

14585
1
SHARE

Inawezekana tatizo halijaanzia hapa. Ila yapo mengi zaidi ya haya ya Yondani. Tusishie kushangazwa na hili la Yondani huku tunafumbia macho yaliyojificha nyuma pazia. Sawa Ni ngumu sana kuamini haya Yondani aliyofanya maan aliwahi kuvaa beji ya unahodha timu ya taifa.

Asante Kwasi sidhani kama timu ya taifa aliwahi kuitwa. Kwasi ameonesha ukomavu wa hali ya juu. Inawezekana kabisa kuna kitu kilimkera Yondani lakini yeye ni Legend.

Ni kweli alikwaruzana na Shafik Batambudze kwenye ishu ya kutemeana mate lakini je nae afanye vile?. Weka nukta hapo
Kilichonifurahisha ni pale refa alipooneshwa mate na Kwasi na bado hakufanya maamuzi, hebu tusikitike…….

Sasa tuendelee.. Lakini kwasi ametupa elimu ambayo Yondani ameshindwa kuwapa Vijana wadogo kama akina Mwishiuya. Yondani alishikwa na hasira sawa, lakini anapswa ajue yeye ni kioo. Sio kombe la Dunia lile. Yeye sio Batambudze. Wapo mashabiki wanataka kubalansi hii habari kufanya ngoma droo. Tena wanataka kuwalaumu Azam Tv kuwa wao ndio waliopaswa kusemelea hilo.

Kwani wakati linatokea wahusika walikuwa wapi? TFF? Je tunyamaze maana amelipiza kisasi?
Au Kigezo ni Mechi ngumu? Maana nimesikia upande wa pili wanadai hivyo!! Yondani amecheza hizo mechi mara ngapi? Kwasi alimkera kivipi? Je ulikuwa ni mzozo mkubwa? Je Kwasi alifanyaje? Labda nimulize Anko Ngasa ambaye nimeona akimtetea Yondani kwenye ukurasa wake wa Instagram?

Kumtemea mtu mzima mwenzio Mate dah? Mate? Yaan ptuuh ya uso? No no! Inasikitisha. Mwanadamu anayeishi unamtemea mate ?unasema ni hasira? Mate? Tena inaonekana yalikusanywa kabisa mdomoni yale!! Hapana ndugu zangu. No no!! Sio sawa! Yondani amekosea mno. Amekosea sana. Amekosea wala tusipepese macho. Hata kama wana yanga mtanichukia ila Yondani ameharibu mno.

Vijana wengi wanatamani kucheza Simba au Yanga. Wapo wanaotamani viatu vya Yondani. Yondani ni mchezaji mzuri lakini bila unafiki nidhamu yake ni mbovuuu. Narudia nidhamu yake ni mbovu sana. Kama kuna wachezaji wachanga watamuiga wasahau kuwa akina Samatta wa kesho. Sio jana tu na sio yeye pekee yake. Hata uwanjani yupo hivo sio yeye pekee yake. Mnakumbuka ishu ya Boban? Wapo wengi. Shida ni Simba na Yanga. Hatuwasemi tunawaogopa. Tunawaogopa kwa sababu wana vipaji. Tunakula chakula kizuri kwenye sahani chafu. Watanzania wengi tunaamini ukicheza mpira kitemi basi wewe unajua. Ujinga huu unapakwa rangi na mashabiki bila kujua madhara yake.
Tusikubali hulka za ajabu ajabu zikateketeza soka letu hili bovubovu. Au mnawaiga akina Suarez na Costa? Wale washafanikiwa. Vile vitimbwi vyao havikosti timu.

Tuachane na hili la Yondani.

Nidhamu ya soka letu ni mbovu sana. Yondani ni mfano tu. Wapo wengi sana. Yondani hajaua amefanya vituko ambavyo vinatokana na nidhamu mbovu ambayo ni adui mkubwa wa soka letu. Nidhamu Ipo chini mno. Ukienda uwanjani Utasikia mashabiki wanakwambia fulani bangi sana. Nani kawaambia mpira ni mchezo wa wahuni? Sina maana kama kuvuta bangi ni uhuni au sio uhuni Wala sitaki kufika huko. Lakini kwa maelezo ya mashabiki ni kwamba mchezaji akionesha nidhamu mbovu ni bangi. Lisemwalo lipo, kama halipo linakuja. Kwenye soka sigara bangi na pombe za kupindukia ni uhuni. Ni upuuzi. Kama wewe ni mchezaji na unataka kufanikiwa na unaendekeza huo ujinga sahau. Hata ligi ya Eritrea hutocheza.
Narudia tena kwenye soka BANGI, SIGARA na ULEVI ni UHUNI. huko kwingine sijui.

Sina maana kwamba Yondani ni mhuni la hasha. Hii nmeongelea kwa wachezaji wote. Hapo mwanzoni kabisa nimetumia Yondani kama kioo cha Nidhamu. Nipate sehemu ya kuliongelea hili.
Samatta yupo Ulaya, unadhani amekwenda ulaya kwa sababu anavutaja sigara na bangi? Juzi nimeona meseji ya mshabiki mmoja kaniambia amemuona mchezaji fulani wa timu fulani yupo mtaani kwao anavuta bangi. Nilitaka kumtaja kwa jina lakini nimepotezea. Sasa unategemea kwa mwendo huu tutafika kweli?.

Ningekuwa kiongozi wa TFF au ngazi yoyote ya kisoka, mchezaji anayejulikana kuvuta bangi au kuwa mlevi hapaswi kupewa kibali cha kucheza ligi kuu. Soka sio genge la kihuni. TFF mpo mnakaa tu. Mnataka kufanya soka letu genge la kihuni. Yaani leo hii unapishana na mchezaji ananuka sigara utadhani umepita karibu na kiwanda cha Sigara. Mtakuja mshikwe shinikizo la damu mtufie uwanjani nyie.
Mpira ni mazoezi kujitunza na kujitambua-Athumani Chuji alisema haya. Chuji huyu huyu ndiye aliyemsifia Yondani kuwa mchezaji bora kwake. Chuji alianza maisha 2003 kipindi kile cha Serengeti Boys, kufikia 2012 yeye pekee ndiye aliyefanikiwa kucheza Vilabu vikubwa wale wengine wote hola. Yondani hawezi kwenda nje tena. Umri ushamtupa mkono. Ana kipaji hasa. Anajua mpira kuliko hata Mavugo lakini hapaswi kuondoka na kioo. Aache vijana wengine wajitazame. Hatuhitaji mate yake, ayatumie mate yake kuhesabia hela.
Sijawahi kuona ulaya mtu ana jicho jekundu kisa bangi. Wachezaji walevi wengi ulaya maisha yao ya soka yaliharibika kama akina Pennant. Mnataka wadogo zenu waige nini? Hata hawa wa U-17 muda sio mrefu nao watajua chocho za kuvuta bangi au kuwa wababe. Soka ni profesheni, hakuna uhusiano wowote wa profesheni na uhuni.
Mnisameheni tu bure, nidhamu ya mpira inaanzia kwenye afya ya mchezaji, akishindwa kuthamini afya yake hawezi kuthamini heshima ya mpira. Nisamehe Yondani kwa kukutumia kama mfano. Umeshindwa kutumika kaa kioo nakutumia kama kichanuo kuchana nywele chafu.


Asante sana Yondani kwa kunipa nafasi kutoa dukuduku nililokuwa nalo muda mrefu nilikuwa natafuta namna ya kuliongelea, bila mate yako nisingeweza kuongea, Asante kwasi kwa kutuonesha profesheno ni nani.
Imeandaliwa na Privaldinho. Mtanisamehe

Comments

comments

1 COMMENT

  1. Nimekubali sana ushaur wako mzur kuhusu soka letu, wachezaji watambue kwamba mpira sio vita, mpira ni burudani, mpira ni ajira, pia kuna maisha baada ya mpira, Leo mchezaji unayemfanyia kitendo kama hicho huyo kesho mnaweza kujikuta mpo timu moja..!!!, je italeta picha gani???? Huwez jua huyo unaemdharau mbelen atakusaidia kwa lipi……….!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here