Home Kitaifa Wanaosema Yanga mbovu Manara anamajibu yao

Wanaosema Yanga mbovu Manara anamajibu yao

12058
0
SHARE

Haji Manara amesema amewasikia baadhi ya mashabiki wa Yanga wakisema timu yao ikiwa mbovu ndio huwa inaifunga Simba, Manara amesema kama wanadhani timu yao ni mbovu wasiipeleke uwanjani kwa sababu hawataki kuifunga timu mbovu.

Anawashangaa mashabiki hao wanao sema Yanga ni mbovu wakati ndio mabingwa watetezi wa VPL wakiwa wameshinda taji hilo mara tatu mfululizo katika misimu iliyopita na kuongeza kuwa hawaidharau.

“Kuna watu nimesikia wanasema Yanga ikiwa mbovu huwa inaifunga Simba, mimi siamini kama Yanga ni mbovu, unasemaje timu mbovu wakati ndiyo bingwa mara tatu mfululizo, wamefuzu hatua ya makundi Afrika. Hata sisi hatutaki kuifunga timu mbovu kama wabovu wasije uwanjani sisi tunataka timu nzuri itupe ushindani watanzania wapate raha.”

“Hatuwadharau Yanga, ni timu bora wamekuwa mabingwa mara tatu mfululizo wameingia hatua ya makundi ya mashindano ya Afrika lakini sisi tunahitaji ushindi. Ushindi wetu utatokana na support ya mashabiki.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here