Home Kitaifa Nyuma ya pazia goli la Erasto Nyoni

Nyuma ya pazia goli la Erasto Nyoni

22371
0
SHARE

Goli la Simba lililofungwa na Erasto Nyoni kwenye mchezo wa watani wa jadi lina siri kubwa kama ulikuwa hujui.

 

Nyoni alitabiriwa na mkewake kuwa atafunga goli dhidi ya Yanga jambo ambalo limetimia, dakika ya 38 kipindi cha kwanza ambapo aliunganisha kwa kichwa mpira uliopigwa na Shiza Kichuya.

Nyoni amemshukuru mkewe na familia yake kwa ujumla baada ya kufunga goli hilo na kuwaomba mashabiki wa Simba waendelee kuisapoti timu hadi ichukue ubingwa.

“Kabla ya mchezo wa leo (dhidi ya Yanga) mkewangu aliniambia nitafunga goli kitu ambacho kweli kimetokea nimefanikiwa kufunga”-Erasto Nyoni.

“Namshukuru mkewangu na familia yangu kwa ujumla kwa kuniombea, nimefurahi timu imeshinda na kupata pointi tatu. Nawaomba mashabiki waendeleea kuisapoti timu hadi tuchukue ubingwa.”

Simba imefikisha pointi 62 baada ya kucheza mechi 26 ikiendelea kuongoza ligi, Yanga inashuka hadi nafasi ya tatu wakiwa na pointi 48 lakini wana mechi mbili mkononi (viporo) nafasi yapili ipo Azam ikiwa na pointi 49 baada ya kucheza mechi 26.

Kimahesabu, Simba imebakiza pointi nne (4) ili kutangazwa mabingwa wapya wa VPL 2017/18.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here