Home Kitaifa Manara akosoa ‘uhasimu’ Simba, Yanga

Manara akosoa ‘uhasimu’ Simba, Yanga

9460
0
SHARE

Kuelekea pambano la Simba vs Yanga leo Jumapili Aprili 29, 2018 Afisa habari wa Simba Haji Manara ametolea ufafanuzi neno ambalo limezoeleka kuitaja mechi hiyo ‘mahasimu’ kwamba si neno zuri na inabidi liepukwe kutumiwa.

Manara amesema Simba na Yanga ni watani wa jadi au wapinzani lakini siku hizi kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiziita timu hizo mahasimu jambo ambalo linajenga picha mbaya kwa mashabiki wapya hasa wa kizazi kipya.

“Hasimu inatokana na neno ‘hasama’  uhasama ni uadui, mahasimu ni kama ilivyo Israel na Palestina, Korea Kaskazini na Kusini, au makundi yanayopigana kule Syria, kwa upande wa vilabu ni kama Gor Mahia na FC Leopards timu ambazo zilikuwa na ugomvi wa makabila mechi ikiisha mashabiki wanakufa kwa mapigano.”

“Mahasimu ni Al Ahly na Zamalek sio watani wale, mechi yao ni vita, wazee wetu wa Simba na Yanga walitengeneza mfumo mzuri sana wakatumia lugha ya ‘watani wa jadi’ ndiyo maana katika historia yetu haijawahi kuchezwa mechi ya Simba na Yanga kukawa na mapigano kati ya mashabiki wa pande mbili hopo pekeyake linaonesha sisi sio mahasimu. Sisi ni watani wa jadi na wapinzani kwenye mpira.”

“Mimi nimeona tuanze kuachana na ile lugha ya mahasimu kwa sababu inajengeka kwa mashabiki wapya wanadhani sisi ni maadui. Nimeshawahi kwenda mahali kuna mtu baada ya kuniona akaanza kunitukana na kunishikia chupa. Lazima tuiondoe tubaki kutaniana na kucharurana hiyo ndiyo raha ya Simba na Yanga.”

“Hakuna haja ya kuonesha kwamba kuna chuki na uadui. Tuna utamaduni wa kufanyiana mema nje ya dakika 90, utamaduni huu tumeukuta hatuwezi kuubadilisha hiyo ndiyo asili yetu Simba na Yanga kwa hiyo tuendele kutumia lugha ya watani wa jadi au wapinzani lakini neno mahasimu nimeomba tuanze kuachana nalo.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here