Home Kitaifa #KuelekeaDarDerby: Wabunge watambiana

#KuelekeaDarDerby: Wabunge watambiana

9001
1
SHARE

Mchezo wa Simba na Yanga unagusa hisia za watu wengi sana ndani na nje ya mipaka ya Tanzania bila kujali vyeo, dini, kabila, vyama vya siasa wala tofauti zao kwa namna yoyote.

Mara nyingi mchezo wa watani wa jadi unapokaribia huwa kunakuwa na tambo nyingi za mashabiki wa timu hizo, hawa ni baadhi ya wabunge Tanzania wenye mahaba na timu zao na wametoa majigambo yao kuelekea mechi ya Jumapili Aprili 29, 2018.

 • William Ngeleja-Mbunge Jimbo la Sengerema

Ukizungumzia soka mimi ni mpenzi na mwanachama wa ‘chama kubwa’ Simba, nafahamu kwamba tar 29 kutakuwa  a shughuli inafanyika lakini nachotaka kusema tunafahamu mikakati iliyopo ni yaushindi.

Dalili zote za Simba kuchukua ubingwa zimeonekana na tunafahamu kwamba tumekuwa na maumivu ya miaka mitano lakini sasa maumivu yetu yamefika mwisho. Kwa pointi ambazo Simba imeizidi Yanga hata kama Simba wakipoteza mchezo huo bado Yanga hawezi kuwa bingwa.

Hatutakuwa sehemu ya Yanga kujifariji wakati anaukosa ubingwa huu, Simba itasimama na itachukua ubingwa.

 • Venance Mhoto-Mwenyekiti timu ya wabunge wa Yanga

Mpira una matokeo matatu, kuna sare, kushinda na kushindwa kwa sababu mimi nimewahi kucheza mpira kikubwa ni timu gani imejiandaa vizuri lakini kwa jinsi ilivyo mara nyingi timu ambayo inakuwa si nzuri sana inakuwa inashinda na mwaka huu Yanga sio nzuri sana naamini itashinda.

Siku zote Yanga ambayo inakuwa si nzuri inaifunga Simba kirahisi kwa hiyo mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi ushindi ni wetu, Simba watalala na viatu.

 • Jumaa Aweso-Mbuge Jimbo la Pangani, Naibu Waziri wa Maji, shabiki wa Simba

Tutashinda kwa kishindo kabisa, mtoto akililia wembe unamwacha umkate, nasema wali wa kushiba unaonekana kwenye sahani na mpaka sasa tunaongoza ligi hakuna wa kutuzuia kwa hiyo ni 3-0 tu, sisi tumeshakuwa mabingwa kwa hiyo tunakila sababu ya shangilia na mashabiki wajitokeze kwa wingi hatuna wa kutuzuia.

 • Ally Hassan King-Mbuge Jimbo la Jang’ombe, shabiki wa Yanga

Kwa upande wetu mchezo umekaa vizuri sana kwa sababu wachezaji wengi waliokuwa majeruhi na hawakucheza mechi za nyuma sasa hivi wamepona na tunatarajia ushindi.

Timu in ari kwa sababu imefuzu hatua ya makundi mashindano ya Afrika kwa hiyo ari hiyo inakuja hadi kwenye mchezo dhidi ya Simba, nafikiri mchezo utakuwa mzuri sana.

Licha ya kocha kuondoka lakini usimamizi upo na mara nyingi timu imeshacheza chini ya kocha msaidizi Nsajigwa na bado ikafanya vizuri kwa hiyo hata mechi hii pia itafanya vizuri.

Siku zote sherehe kubwa huwa pale mtu anapooa bikra kwa hiyo na sisi tunaenda kuoa mwanamke ambaye hajawahi kuwa mtu mzima, sisi ndio tutamkomaza.

Comments

comments

1 COMMENT

 1. I often visit your blog and have noticed that you don’t update it
  often. More frequent updates will give your page higher authority & rank in google.
  I know that writing content takes a lot of time, but you can always
  help yourself with miftolo’s tools which will shorten the time of creating an article to a couple of seconds.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here