Home Kitaifa Mshabiki wa Simba amuonya Chirwa

Mshabiki wa Simba amuonya Chirwa

11555
0
SHARE

KELVIN RICHARD MKARUKA, MPWAPWA.

Mimi ni shabiki mkubwa wa simba, naishauri timu yangu itakapoingia kesho uwanjani icheze kwa kujiamin ila isijiamin kupita kiasi kwa kuwa Yanga nayo ni timu kubwa, na wacheze kwa nidhamu kubwa sana ili kuepuka adhabu zinazoweza kuigharimu timu. Pia wachezaji wawe makini sana kwa maana tukishinda kesho tutakua katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa tulioukosa kwa mda mrefu.

James Simon Yulamas , Sumbawanga.

Naiombea timu yangu SIMBA iweze kuibuka na ushindi mnono. Vile vile Chirwa asije akawa Kane wa Tanzania, akasema magoli ya Okwi ni yake huwa anayaparaza weeeeee! Chirwa rudi kavune mahindi yako yashakoma..!

Naitwa Ramadhan Rashi, Uvinza, Nguruka kata ya bweru.

Nauliza je, Niwachezaji gani wa Yanga ambao hawata kuepo katka game ya Simba na Yanga.?

Naitwa Isack kalinga, Dodoma
Mshabiki wa Simba mimi ningemshauri huyu kocha wa Simba juu ya uwepo wa viungo washambualiaj asilia uwanjani kama Mzamiru na Ndemla inaweza kusaidia kuleta matokeo tofauti na hivyo itakuwa na hatari katikati yetu kwan mfumo wa kuweka mabeki watatu wa kati n kama kubaki basi kitu ambacho kinaondoa dhana halisi ya Barca ya bongo!!! Simba nguvu moja.

Naitwa said issa, koani Zanzibar
mtazamo wangu katika mchezo wa watani wa jadi hapo kesho mechi itakua ngumu kwasababu mechi kama hizi timu ambayo haina matokeo mazuri katika michezo yake huwa na asilimia kubwa ya ushindi ushauri wangu kwa timu zote mbili ziende uwanjani kwa kutupa burudani mashabiki zao tunataka kuona mpira sio maneno katika vyombo vya habari.

Naitwa TUSEKELE CHOMO, ISOKO, ILEJE SONGWE.
Wanaoibeza YANGA Hawazijui Mechi za Watani wa Jadi Mechi hizi hazizingatii Ubora wa Timu, bali nafasi upatazo

Naitwa Kaitani Tarimo, Usseri rombo.

Ushindi kwa mnyamaaaa chura aende zake bondeni kule kuogelea.

Aziz Mtambo, Dar

Yanga wanahitaji kuwa makini zaidi eneo la kiungo kwa sababu msimu huu tumeshuhudia Simba magoli mengi yananzia katikati na kupeleka pembeni wamekuwa wakicheza kitimu eneo hilo me nafikri kama Yanga atahitaji ushindii ajarbu kuwin eneo la kati la Simba ningependa hyo game Kamusoko na tishishimbi waanze eneo la kiungo

Best Anania, Mbeya

Mimi mshabiki wa yanga damu yanga wakaze tu hakuna okwi bocco wala kuchuya,yondani ninja fanyeni wajibu wenu wanayanga tupo nyuma yenu.

Naitwa Nada, Ndago singida,
shabiki wa simba nisiye kuwa na presha,
ninacho shauri ni kwamba wasimdharau mpinzani wake, kwani zinapo kutana timu hizi mechi inakuwa ngumu hata kama mwenzako anakuwa na madhaifu basi siku hiyo ana kamilika. KILA LA KHERI MYAMA SIMBA KWENYE MAWINDO YAKO.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here