Home Kitaifa Mambo ya Watani: Ajibu Mapema sana, Huyo Tshishimbi sasa

Mambo ya Watani: Ajibu Mapema sana, Huyo Tshishimbi sasa

10478
0
SHARE

Naitwa Athuman lichonyo, Lindi, Nachingwea
Nachowaomba wachezaji wa yanga wacheze kwa kujiamin irikesho tutoke naushindi.

Martin Buluba, Arusha
Yanga wanapaswa kuwa na makink eneo la katikati kwa siku za karbuni Simba wameonkana kufeli sana eneo hilo. Ushindi wa simba unatokea zaid kwenye mbavu,,(wings) hilo lilikuwa wazi zaidi kwenye mechi mbili za mwisho.

Naitwa Hamisi Yusuf Killo.
Mimi ni shabiki wa Simba kimtazamo mechi itakuwa ngumu kwa upande wa Yanga sababu wana kocha ambae hajamaliza hata wiki tangu aanze kuwafundisha je mfumo ambao amefundisha ushanza kufiti katika kikosi changa kikubwa wakubali ya kwamba msimu huu wamepoteza wampe kocha muda aijenge Yanga ili ilete ushindani kwa mnyaaaaaama msimu ujao mwaka huu vyura wahamie vumbini kuongelea

Moses, Sumbawanga
Mimi ni mshabiki wa Yanga damu me nadhani wanoibeza Yanga hawajui Yanga ilivyo me nashauri kocha wa Yanga mbele amuanzishe Chirwa Ajibu Mhilu naamini Simba watakaa maana wanaweza kuwa na gari lenye sula nzuri halafu me nikawa gari lenye sura mbovu tukafika mliman mimi nikapanda wewe ukashindwa kupanda

SALIM ROMANO, Sumbawanga
Mimi ni Simba damu, ninachoomba kwa makocha wa timu zote mbili wapeleke timu uwanjani zikafunguke zikacheze zisilinde namini tutashuhudia burudani na raha ya soka magori.kama kawa kesho Simba 3 vs Yanga 1

SALUM JUMANNE, KALIUA-USINGE
Napenda kushauri bench la ufund la simba wasidharau mechi waweke fulu mziki maana yake alama 3 ni muhimu sana.

Benny, Geita,
Timu yangu SIMBA ili ishinde inabidi icheze Mpira wa kasi mwanzo mwisho, isije ikapata goli moja ikaridhika na kupunguza kasi mnyamaa oyee!

Mustaf Rashid, Kibaha
ushauri wangu kwa simba wasibweteke na upana wakikosi kwani mchezo huu hautabiliki lakini Simba naipa nafasi kubwa yaku shida ikichagiwa nasafu yaushambuliaji Okwi Bocco Kichuya

Mimi Gadson J, Kigoma
Simba ni timu nzuri tatizo lao ni presha wanapokutana na watani wao, ushauri wangu waache hofu wapige mpira ushindi lazima.

Emanuel Bonifasi, Singida
Kwa Mechi Ya Kesho Ni Ngumu Kutabri Japo Simba Mwaka Huu Wako Vizuri Lakni Mpira Dakika Tisini Kila Timu Ina Nafasi Ya Kushinda Yanga Au Simba Na Inategemeana Na Upangaji Wa Kikosi Mzuri

Uswege Bakegamo (mbotika) Mbeya.
Sawa gem litakuwa gumu. lakini sijaona wa kumzuia okwii boco.

Muhidin kipote, Mbuchi kibiti
Mimi ni mshabiki wa Yanga nachotaka kesho Tshishimbi anzie juu yani namba 8 sita makapu basi hao simba mapema Ajib Chirwa fanyeni yenu taifa kesho timu makini uwongozi makini

Mdau wa Simba

Mimi napenda niseme kikosi changu ni manula, Kapombe, kwasi, mpilipili, Nyoni, Mkude, Kichuya, Mzamiru, Okwi, Mavugo, Ndemla. Ukiangali kikosi hiki kila mmoja anauwezo wa kukaa na mpira, hiki ndio kitawapoteza Yanga. Yanga ikikutana na timu inayocheza mpira mwingi wanapotea. Ukipija goli mbili, unatoa Ndemla unaingiza Kotei, unatoa Mavugo unaingiza Juuko hapo unatulia unaangalia nani tena kapotea ili ufanye Sabu ya mwisho.

Asanteni wadau wote. Kaa hujaona Meseji yako hapa usijali tupo pamoja tutaendelea kuwapa uwanja mashabiki nanyi mtoe uchambuzi wenu. Imeandaliwa na Privaldinho unaweza kunifollow instagram kwa jina hilo hilo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here