Home Kitaifa #KuelekeaDarDerby: “Sioni beki wa Yanga wa kumkaba Okwi na Bocco

#KuelekeaDarDerby: “Sioni beki wa Yanga wa kumkaba Okwi na Bocco

10093
0
SHARE

Mchezaji wa zamani wa Simba pia amewahi kuifundisha timu hiyo kwa nyakati tofauti kocha Jamhiri Kihwelu ‘Julio’ anatamani Simba ipate ushindi Yanga siku ya Jumapili Aprili 29, 2018 ili kujihakikishia ubingwa wa ligi msimu huu.

Julio amesema kwa sasa haoni beki wa Yanga ambaye anaweza kuwazuia washambuliaji wa Simba Emanuel Okwi na John Bocco ambao wapo kwenye ubora wao wa kutupia kambani.

“Upande wangu napenda tuwafunge Yanga kwa sababu naamini tukishawafunga tayari tunakuwa mabingwa, lakini kama watatufunga wataanza kutuletea ugumu kwenda kwenye ubingwa.”

“Si dhani kama kuna beki kwa kipindi hiki wa kuweza kumkaba Okwi au John Bocco wengine sitakikuwasema mambo ni mepesi yanaeleweka.”

“Yanga wajipange, tupo vizuri sidhani kama kipindi cha kwanza watamaliza hawajachezea tatu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here