Home Kitaifa #KuelekeaDarDerby: Mpira una majina yake, ‘Ninja’ kwenye sinema”-Julio

#KuelekeaDarDerby: Mpira una majina yake, ‘Ninja’ kwenye sinema”-Julio

11138
0
SHARE

Huyu kocha Julio ana mineno bwana! Wakati anawasifia washambuliaji wa Simba Okwi na Bocco kwamba haoni beki wa kuwazuia kwa upande wa Yanga, Mkazuzu akamuuliza vipi kuhusu Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambaye siku za karibuni ameonesha kiwango kizuri?

Majibu ya Julio ndio yanaweza kukuacha hoi, eti anasema majina mengine anezoea kuyasikia kwenye movies ila sio uwanjani, yani akimaanisha Ninja ni jina la kwenye movie. Halafu anasema eti Yanga wameshazoea majina ya ajabu tangu kitambo sana kwa hiyo hashangai sana kusikia mchezaji anaitwa Ninja.

“Unajua mpira una majina yake, mpira majina yake Messi, Ronaldo, Yanga tabia hii ya majina ya ajabu wanayo tangu siku nyingi kuna watu walikuwa wanaitwa Scania, Tata, kama hivyo Ninja hao wote wanapatikana kwenye sinema.”

“Lakini kwetu kule sisi utasikia Messi kwa hiyo watu wa mpira wapo majina ya sinema yapo Yanga kwa hiyo kama ni sinema watatushinda.”

“Siku zote masikio hayazidi kichwa, naamini Simba tutaibuka na ushindi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here