Home Dauda TV #KuelekeaDarDerby, Kibaden afunguka kuhusu nani anaweza kuvunja rekodi yake ya “hattrick”

#KuelekeaDarDerby, Kibaden afunguka kuhusu nani anaweza kuvunja rekodi yake ya “hattrick”

12546
0
SHARE

Jina la Abdalah “King” Kibaden sio jina geni kwa washabiki na wapenzi wa soka nchini, jina la Kibaden linazungumziwa sana haswa wakati wa pambano la Simba na Yanga hii ni kutokana na rekodi aliyoiweka mwishoni mwishoni mwa miaka ya 70 ya kufunga hattrick katika mchezo wa Simba vs Yanga.

Timu ya ShaffihDauda.co.tz na Dauda Tv ilikwenda kumtembelea King nyumbani kwake kujua machache kuhusu rekodi yake na mtazamo wake kuelekea Kariakoo Derby kati ya miamba miwili mikubwa ya soka nchini Tanzania Simba vs Yanga.

Kwanza Dauda Tv ilitaka kujua nini kilitokea wakati King akiifunga Yanga hattrick “tulikuwa na hasira sana ile siku, mashabiki wa Yanga walituzomea sana siku moja tukiwa kwenye basi(siku chache kabla ya mchezo), nakumbuka baada ya kutuzomea tulichukua mazoezi hadi usiku ili kuikomesha timu yao”

Kibaden anasema hasira zile ndio zilimpelekea kuwafunga Yanga mabao matatu siku hiyo, hapohapo linanijia swali kuhusu vijana wa sasa ambapo nilimuuliza Kibaden kama kwanini rekodi imekuwa ngumu kuvunjika na anaona nani anaweza kuivunja katika mchezo wa Simba vs Yanga.

“Mimi nilikuwa na malengo mengi kitu ambacho vijana wa sasa hawana na ndio maana inakuwa ngumu kuivunja rekodi yangu, lakini kwa sasa ukiwaangalia John Bocco na Okwi wanaonekana kucheza vizuri na ni vijana wanaoonekana kuwa na malengo, haswa Okwi” Japokuwa King hakuweka wazi kuhusu nani atavunja rekodi yake lakini anaonekana wazi kuukubali mziki wa Bocco na Okwi.

Katika kuelekea Yanga vs Simba, Kibaden anaamini Simba wana uwezo mkubwa sana kwa sasa na bila kupepesa macho anawapa nafasi Simba kutokana na namna ambavyo kikosi chao kimekuwa kikicheza msimu huu tofauti na mahasimu wao wakubwa Yanga, hii hapa Interview na Kibaden

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here