Home Kitaifa #kuelekeaDarDerby: Wasemavyo wafanyabiashara

#kuelekeaDarDerby: Wasemavyo wafanyabiashara

11034
0
SHARE

Jumapili Aprili 29, 2018 itachezwa mechi ya Simba na Yanga mechi ya pili katika msimu wa ligi 2017/18 inayotarajiwa kuchezwa uwanja wa taifa.

Pindi timu hizo zinapokutana mambo mengi huwa yanatokea ndani na nje ya uwanja, ikiwemo tambo za mashabiki, ahadi mbalimbali mambo ambayo huongeza ladha ya mchezo huu.

Licha ya burudani inayopatikana kupitia timu hizo, wafanya biashara mbalimbali wanaofanya biashara pembezoni mwa iwanja unaotumika wamekuwa wakinufaika kutokana na idadi kubwa ya mashabiki wanaojitokeza kushuhudia mchezo huo.

Sports Xtra imefanya ziara katika uwaja wa taifa ambao utakuwa mwenyeji katika ujao wa Simba vs Yamga siku ya Jumapili na kuzungumza na wafanya biashara mbalimbali wakieleza wanavyonufaika na mchezo huo ukilinganisha na miaka mitatu iliyopita.

Omary Mbegu-muuza jezi 

Mauzo ya Simba na Yanga kwa sasa yameshuka tofauti na zamani ambapo mwamko ulikuwa mkubwa sana, kipindi hiki unakuta kuna foleni hapa watu wananunua jezi lakini siku hizi hadi saizi bado hujauza jezi hata moja kwa sababu mapenzi na hizo timu yamepungua sana hata ujaji wa mashabiki uwanjani umepungua.

Hata upatikanaji wa tiketi zamani na sasa ni tofauti, siku hizi mtu anasumbuka kupata tiketi anaweza akatoka nyumbani akaja hadi uwanjani akazungushwa kupata tiketi matokeo yake anaamua kurudi nyumbani.

Anaepata tiketi anaweza kupata mtihani wa kuingia uwanjani, unaambiwa mashine zinasumbua kwa hiyo usumbufu kama huo unapelekea mwamko wa watu kuja uwanjani unapungua matokeo yake watu wengi wanaamua kubaki nyumbani kuangalia mpira kwenye TV.

Kwa hiyo hata uuzaji wa jezi umekuwa mdogo tofauti na zamani. Zamani mechi ya Simba na Yanga unaweza kuuza hadi zaidi ya jezi 100 lakini siku hizi hata jezi 50 huwezi kuuza, ukiuza sana basi jezi 30.

Said Kiwele-Bodaboda 

Kwa kipindi hiki chote biasharabya bodaboda imebadilika, imekuwa ngumu lakini siku ya mechi ya Simba na Yanga kidogo biashara inachangamka tunaokotaokoto kidogo.

Mashabiki wanaoongoza kupanda bodaboda ni wa Yanga, hata kama watakuwa wachache wakitoka uwanjani wanazagaa maeneo ya hapa gari zinakuwa zimeshakata kwa hiyo sisi tunafanyabnao biashara.

Chid Somboko-mmiliki Stadium Bar, uwanja wa taifa 

Mechi ya Simba na Yanga inakuwa kama sikukuu, watu wengi utaona wanapita wengine wanafanya biashara mbalimbali, wauza bazoka, karanga, wauza vyakula wanakuepo pia wengi.

Mauzo yanakuwa mazuri ndio maana nikasema inakuwa kama sikukuu, watu wanapanga bidhaa zao wanaendelea na biashara. Maandalizi kuelekea mechi hii yanakuwa tofauti na nyingine.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here