Home Kitaifa #KuelekeaDarDerby: Pawasa kaipa ushindi Simba

#KuelekeaDarDerby: Pawasa kaipa ushindi Simba

10551
0
SHARE

Beki wa kati wa zamani wa Simba Boniface Pawasa pamoja na mambo mengine lakini bado ameipa nafasi klabu yake ya zamani kushinda mchezo wa watani wa jadi ‘Kariakoo derby’ siku ya Jumapili.

Pawasa ambaye alikuwepo kwenye kikosi cha dhahabu cha Simba kilichoivua ubingwa wa Afrika Zamalek ya Misri amesema, anaipa Simba nafasi kwa sababu ya takwimu zake nzuri za mechi zilizopita tangu kuanza kwa msimu huu.

“Ukiangalia mechi za mwisho timu zote zimekuwa na uwiano sawa wa kupatabmatokeo lakini kabla ya hapo kila timu imekuwa na mfululizo mzuri wa kushinda mechi zake.”

“Wasiwasi wangu ni ujio wa kocha mpya wa Yanga na kuanza kibarua chake mapema sana. Kwa ninavyoelewa walimu wanakuwa wanatofautiana falsafa kitu ambacho kinaweza kupelekea wachezaji kushindwa kuendana na mfumo au style ambayo yeye atataka kuitumia ndani ya muda mfupi.”

“Jambo zuri ni kwamba bado Nsajigwa na yule kocha mwingine (Noel Mwandila) wapo na ni watu wenye weledi na ufahamu mkubwa wanaweza kumshauri kocha mpya ni jinsi gani ya kuiingia mechi ya Simba na Yanga.”

“Lakini niseme kweli, naiona Simba ina kikosi kizuri safu nzuri ya ushambuliaji inayowapa magoli mengi ukilinganisha na Yanga lakini hilo halimaanishi kwamba mechi imeisha.”

“Cha msingi ni kwamba haitakiwi tiimu yoyote kwenda uwanjani ikiwa na matokeo mkononi, mpira wa Simba na Yanga inaingia kwenye vitabu vya historia kwa hiyo ina umuhimu wake hata ukiangalia maandalizi yake ni tofauti kabisa.”

“Ni mechi ambayo inaweza kuharibu maisha ya wachezaji kama utaboronga au kucheza vibaya unaweza kupotea kwenye ramani ya mpira lakini kama utang’aa ukapata kitita kinene wakati wa usajili.”

“Kwa upande wangu karata yangu naipa Simba kwa sababu ya takwimu za mechi zilizopita.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here