Home Kimataifa #KuelekeaDarDerby: Mtazamo wa Dr. Tiboroha “mechi ipo wazi”

#KuelekeaDarDerby: Mtazamo wa Dr. Tiboroha “mechi ipo wazi”

11221
0
SHARE

Kuelekea pambano la Simba vs Yanga, Katibu wa zamani wa Yanga Dkt. Jonas Tiboroha ametoa mtazamo na maoni yake kuhusu mchezo huo wa Jumapili ya Aprili 29, 2018.

Dkt. Tiboroha watu wasiichukulie poa Yanga kutokana na kuwa na wachezaji wake wengi kubwa majeruhi kwa sababu imeweza kufanya vizuri ndani na nje ya nchi huku wachezaji wake wa kutegemewa wakiwa nje ya uwanja.

“Huu mchezo bado nauona upo wazi timu yoyote unaweza ikashinda mchezo huo japokuwa Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa haina matikeo mazuri sana katika ligi ukiachana na mashindano ya kimataifa.”

“Yanga wametoka kupata sare dhidi ya Mbeya City na Simba walitoka sare na Lipuli lakini ukiagalia performance wise Simba wako vizuri kidogo ukilinganisha na Yanga.”

“Naiona hii mechi ipo wazi kwa sababu ya kitu kimoja, nafasi inaweza kutokea Simba kwa sababu wapo vizuri wanapata ushindi mara nyingi wanafunga magoli mengi kwa hiyo wakaja kwa kujiamini kupita kiasi na kutoipa umakini mechi inayokuja kitu ambacho kinaweza kuwasaidia Yanga wakapata matokeo.”

“Yanga kwa upande wao ni timu ambayo imefanya vizuri  na wamepata matokeo kwenye mazingira magumu, wachezaji wao wengi hawapo vizuri kutokana na majeraha.”

“Juzi kwenye mechi dhidi ya Mbeya City Kelvin Yondani pia alipata majeraha kwa hiyo ni timu yenye majeruhi wengi sana. Sitegemei na sijui kama wachezaji wenye majeruhi wanaweza kucheza mechi ijayo.”

“Watu wanaweza kufikiri kwa kuwa Yanga inakuja huku wachezaji wake wengi wazuri na wakutegemewa wakiwa wako nje mechi inaweza kuwa rahisi lakini wasiibeze Yanga kwa sababu pamoja na kuwa wachezaji wengi wapo nje bado inafanya vizuri katika mashindano yake ya ndani na nje.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here