Home Ligi EPL Eti Mourinho hashindagi big mechi?

Eti Mourinho hashindagi big mechi?

11129
0
SHARE

Na Priva ABIUD

Ndani ya wiki saba Mourinho amebadili hali ya hewa. Amenyamazisha yale makelele yaliyokuwa yanaendelea kuhusu uwezo wake katika mechi kubwa. Msimu uliopita rekodi ya Jose ya mechi kubwa ilikuwa na mbovu sana. Ilikuwa aibu hata kuhadithia. Aliokota kagoli kamoja tu katika michezo 8 ya ugenini. Mourinho hakuwahi hizi siku za nyuma.

mnamo tarehe 18 September 2012 katika michuano ya UEFA Champions League kati yaReal Madrid v Manchester City

Hapo awali amekuwa na sifa ya kushinda michezo migumu kushinda kocha ya yeyote ndani ya ligi kuu England. Na hii ndiyo ilimpa Mou jina kubwa sana. Alijulikana kama Special One. Hili jina hakupewa hovyo hovyo. Ila ubabe wake wakupata matokeo kwenye michezo hatatishi. Kwenye msimu wake wa kwanza klabuni Chelsea alipoteza michezo 5 tu kwa kipindi cha miaka 3 dhidi ya timu zilizokuwa zikishikilia nafasi 4 za juu.

Kwenye msimu wake wa kwanza Porto alishinda michezo yake ya nyumbani yote ya dhidi ya timu 6 za juu na kushinda kwa asilimia 70 ya michezo yote kwa ujumla dhidi ya timu hizo. Akiwa Chelsea alishinda kwa asilimia 63 ya michezo yote ya Big 6 katika uwanja wa Stamford na mwaka uliofuata ilipanda kwa asilimia 75.

Msimu huu vipi?

Man United 2-1 Chelsea
Ilikuwa vita ya nafasi ya Pili. Mourinho na Antonio Conte walikutana tena kwa mara nyingne huku vita yao ya maneno ikiwa imefika patamu.

Vita ya meneno ilitazamiwa sana. Walio wengi walikuwa wakisubria kama Mou na Conte watashikana mikono.

Wakati huu wote waliweka pembeni chuki zao na wakasalimiana bila tabu. Ndiyo.

Wanaume wanapaswa kuwa hivyo bifu ni mambo ya kizamani hayo.

Willian aliwatanguliza wazee wa darajani mbele kunako dk ya 32 kabla ya Lukaku kukomboa dk 39 na Jese Lingard kupeleka kilio kunako dk ya 75. Hapo awali kabla ya mchezo huo kikosi cha Mashetan wekundu kilikuwa na rekodi mbovu ya kufunga goli zaidi moja kwenye mchezo mmoja tu kati ya michezo 7 katika uga wa Old Trafford dhidi ya timu za top 6. Conte nae alikuwa na rekodi nzuri ya kushinda michezo 3 kati ya mine dhdi ya Mourinho.

Man United 2-2 Liverpool
Ni mechi ambayo ililalamikiwa sana na wadau wengi wa soka hasa wale ambao sio mashabiki wa Man United. Huenda makelele hayo hayamsumbui sana Mou hasa baada ya kutoa kipigo cha mabao mawili kwa moja.

Jambo la kujivunia kwa kikosi cha Man United ni kuhakikisha kuwa Sio Mo Salah, wala Sadio Mane au Roberto Bobby Firmino waliotikisa nyavu zao. Rashford alitikisa nyavu mara 2 kabla ya Eric Baily kujifunga kunako dakika ya 66.

Manchester City 2-3 Manchester United
Ulikuwa wakati muafaka wa Paul Pogba kuonesha ulimwengu kwamba hakuna Pogba wa Juve wala wa Yanga. Baada ya Deschamps kusema kuwa Pogba hana furaha, hakusita kuitafuta furaha ambayo ilionekana kusinyaa.

Paul Pogba, akishangilia bao lake dhidi ya Manchester City katika uwanja Etihad jijini Manchester, April 7, 2018.

Magoli yake mawili katika mchezo ambao Man City walikuwa wanahitaji alama 3 kuwa mabingwa yalitibua sherehe yao. Magoli la Vicent Kompany, pamoja na Ilkay Gundogan yalionekana kama tiketi ya ubingwa wao wa 3. Mambo yaliharibika kipindi cha pili pale Smalling alipoibuka shujaa mnamo dakika ya 69.

Guardiola aliwaweka benchi baadhi ya wachezaji wake muhimu mara bada ya kupokea dozi ya mabao matatu kutoka kwa majogoo wa jiji la Liverpool ili kuwapumzisha kwa mchezo uliofuta. Mchezo huu ulikuwa mgumu sana kama kawaida ya Michezo ya Pep na Mou kwani kadi za njano zilikuwa 9.

Tottenham 1-2 Man United

LONDON, ENGLAND – JANUARY 31: Phil Jones wa Manchester United na Harry Kane of Tottenham

Huu ni ushindi wa 3 ugenini kwa Jose Mourinho kwa zile timu kubwa 6. Shukran zote zitamwendea Ander Herrera ambaye msimu huu amekuwa na wakati mgumu sana hasa baada ya ujio wa Namanja Matic na kupandishwa kwa kijana mdogo Scott Mc tominay.

Huenda huu ukawa msimu mwingine ambao Man United hawatatoka kapa mara baada ya Van Gaal kuwapa FA, Mourinho msimu uliopita kutwaa Europa na kombe la ligi. Huu ni ushindi wa wapili msimu huu kwa Mourinho dhidi ya Tottenham kati ya michezo mitatu.

Jose Mourinho akiwa amebeba English League Cup February 26, 2017.

Imeandaliwa na Privaldinho. unaweza pia kunifollow Instagram kwa jina hilo hilo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here