Home Kitaifa #KuelekeaDarDerby: “Waamuzi hawajabadilishwa”-Mwenyekiti kamati ya waamuzi

#KuelekeaDarDerby: “Waamuzi hawajabadilishwa”-Mwenyekiti kamati ya waamuzi

11496
0
SHARE

Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi ndani ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) Salum Umande Chama amesema waamuzi waliopangwa kuchezesha mchezo wa watani wa jadi Simba vs Yanga hawajabadilishwa kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Chama amewataja waamuzi ambao watasimamia mchezo huo utakaochezwa Jumapili Aprili 29, 2018 kwenye uwanja wa taifa.

“Waamuzi tuliowapanga hawajabadilishwa ni walewale, mwamuzi wa kati ni Emanuel Mwandembwa (Arusha), line one Frank Komba (Dar), line two Mohamed Mkono (Tanga) na fourth official ni Hery Sasii”-Salum Umande Chama.

“Hawa ni waamuzi wa kimataifa ukizingatia kwamba Emanuel Mwandembwa amepata badge ya Fifa msimu huu kwa sasa yupo Burundi anachezesha mashindano ya U17 Burundi.”

“Mohamed Mkono pia amepata badge ya Fifa msimu huu na yeye yupo Burundi anachezesha mashindano ya Caf.”

“Frank Komba ni mwamuzi mzoefu kwa hiyo naamini watachezesha vizuri na mshindi atapatikana kwa njia halali.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here