Home Kitaifa Shaffih Dauda ampa Salah Ballon d’Or

Shaffih Dauda ampa Salah Ballon d’Or

12205
0
SHARE

Kutokana na kiwango bora anachoendelea kuonesha mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah kwenye mashindano mbalimbali msimu huu, mchambuzi wa masuala ya michezo Shaffih Dauda amesema kijana huyo wa Misri anastahili kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Dunia maafuru kama Ballon d’Or.

Dauda amefika mbali zaidi na kusema kwa kiwango cha Salah katika msimu huu ni zaidi ya wakali wawili duniani Ronaldo na Messi.

“Kwa sasa nafikiri Mo Salah yuko kwenye kiwango bora zaidi ya Messi na wachezaji wengine hata Ronaldo kwa sababu Ronaldo na Messi ndio wachezaji wanaozungumzwa sana.”

Tuzo ya mchezi bora wa Dunia Ballon d’Or wanasema ni nani wa kwenda kuungana na Ronaldo na Messi kwa sababu wao tayari majina yao yako pale kwenye hiyo tuzo, mwingine ni nani anaekwenda kuungana nao kuwania tuzo hiyo?

Dauda anasema, Mo Salah siyo tu anakwenda kukamilisha idadi ya wachezaji watatu wanaoingia fainali kuwania tuzo ya Ballon d’Or msimu huu bali ni akina nani wanakwenda kuungana na Salah kuwania tuzo ya Ballon d’Or.

“Namuweka Mohamed Salah namba moja kwenye tuzo ya Ballon d’Or halafu tutafute wengine wa kuungana nae”-Shaffih Dauda.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here