Home Kimataifa “Roberto Firmino watu hawamwangalii wala kumzungumza kabisa”-Ruge Mutahaba

“Roberto Firmino watu hawamwangalii wala kumzungumza kabisa”-Ruge Mutahaba

13975
0
SHARE

Jana usiku Liverpool ilishinda 5-2 dhidi ya AS Roma kwenye usiku wa Ulaya, magoli ya Liverpool yalifungwa na Mohamed Salah (alifunga mawili), Roberto Firmino (alifunga mawili) na Sadio Mane akafunga goli moja.

Ruge Mutahaba anaamini mafanikio ya Liverpool yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na Firmino ingawa watu hawamwangalii kwa ukubwa ambao wanazungumzwa wachezaji wengine kama Mo Salah kwa sababu anafunga kila siku.

“Roberto Firmino watu hawamwangalii wala kumzungumza kabisa, lakini nafikiri ndiyo mtu muhimu kuliko watu wanavyofikiri”-Ruge kuhusu mchango wa Firmino ndani ya Liverpool na mafanikio ambayo inayoyapata.

Mjadala huu umekuwa mkubwa kwa wadau wa soka hasa kuhusu Firmino kutopewa nafasi ya kutosha kwenye timu ya taifa ya Brazil katika harakati zake kuelekea kombe la Dunia.

Baada ya Liverpool kufunga goli la pili katika mchezo wa UEFA Champions League dhidi ya AS Roma na ubao kusomeka Liverpool 2-0 AS Roma, Ruge ambaye ni shabiki wa kutupwa wa ‘majogoo wa jiji’ alimpigia simu Shaffih Dauda na kumwambia wakati mwingine furaha ya kipindi cha kwanza inatosha hata kama hautofurahia hadi mwisho wa mchezo.

“Furaha ya kipindi cha kwanza (half time) wakati mwingine inatosha hata kama hautofurahi hadi mwisho wa mchezo”-Ruge, baada ya Liverpool kuongoza 2-0 dhidi ya AS Roma hadi wakati wa mapumziko katika mchezo wa vilabu bingwa Ulaya Aprili 24, 2018.

Ni matokeo ambayo yaliwafanya mashabiki wa Liverpool wahisi kama wapo nchi ya ahadi kutokana na furaha waliyokuwa nayo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here