Home Kitaifa Mbeya City yafafanua ‘utata’ mechi vs Yanga

Mbeya City yafafanua ‘utata’ mechi vs Yanga

11733
0
SHARE

Baada ya kutokea tafrani na vitimbi vilivyoambatana na malalamiko kutoka kwa timu za Yanga na Mbeya City, uongozi wa Mbeya City umetolea ufafanuzi kilichotokea kwenye mchezo huo uliofanyika uwanja wa Sokoine Mbeya.

Mtendaji wa Mbeya City Emanuel Kimbe amesema, kinachozungumzwa myaani ni tofauti na hali halisi ilivyokuwa.

“Baada ya mchezo wa juzi jana tumefanya uchambuzi wa kutosha kwenye maeneo yote, hatukuoshia kupitia picha za video ambazo tulipewa DVD na Azam TV. Tumehoji baadhi ya wachezaji na benchi la ufundi kwamba nini kilitokea.

“Mwamuzi Shomary Lawi hakuutendea haki mchezo wetu kwa bahati mbaya sio mara ya kwanza kuharibu mchezo wetu. Mwamuzi alikataa penati ya wazi baada ya mpira kuzuiliwa kwa mkono na Gadiel Michael, hata Gadiel kwa lugha ya picha alikubali ile ilikuwa ni faulo.

“Dakika 10 baadae akatoa adhabu ndogo ua Juma Mahadh na Hassan Mwasapili ambapo Mahadh alimshika shati Mwasapili na akatereza mwenyewe, line one akaonesha ni faulo mwamuzi alikuwepo eneo la tukio atatoa adhabu ndogo iliyozaa goli.

Kimbe amefafanua kuhusu malalamiko kwamba mchezaji wao aliingia uwanjani licha ya kutolewa nje ya uwanja kwa ajili ya kufanyiwa matibabu.

“Dakika ya 65 tukapata kadi nyekundu ya Ramadhani Malima ambaye alitoka uwanjani na kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo mchezo ukaendelea tukiwa pungufu.

“Tukapata goli dakika ya 90+1 tukiwa pungufu wakati huo mwamuzi alishaonesha dakika sita za nyongeza, dakika ya 95 aliumia golikipa wetu Owen Chaima, wakati Chaima ameumia Daudi Ambokile nae alikuwa amegongwa kwa hiyo benchi la ufundi likampumzisha Ambokile dakika ya 96  ambaye alitolewa nje ya uwanja kwa machela.

“Mabadiliko hayo mwamuzi aliyaridhia, wakati mwamuzi anaangalia nani anaetoka, nahodha wetu Hassan Mwasapili akamwonesha anaetoka ni Ambokile ambaye anatolewa nje ya uwanja mwamuzi akaridhia Daniel Joram akaingia.

“Baada ya Ambokile kutibiwa hakuwa ameona kwamba amefanyiwa mabadiliko, line two akamuuliza unaweza kuendelea akasema ndio, mwamuzi akamruhusu aingie dakika ya 97.

“Kocha Nswanzurwimo alikuwa mtu wa kwanza kuona hilo tukio, ukiangalia video utaona anatoka kwenye eneo lake anakwenda kwa line one kumwambia mwamuzi amemruhusu Ambokile ambaye tayari alishafanyiwa mabadiliko.

“Wakati Nsajigwa anakwenda kulalamika kwa fourth offocial tayari kocha wetu alishamwambia amwambie mwamuzi asimamishe mchezo kuna mchezaji yupo uwanjani kinakosa.

“Ambokile alikaa uwanjani kwa sekunde 42 akatoka uwanjani mwenyewe baada ya kuambiwa ameshafanyiwa mabadiliko, baada ya kutoka mwamuzi akamaliza mchezo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here