Home Kitaifa #KuelekeaDarDerby: Simba, Yanga zagongana Moro

#KuelekeaDarDerby: Simba, Yanga zagongana Moro

10877
0
SHARE

Baada ya klabu ya Yanga kuwasili mjini Morogoro siku ya Jumatatu, Jumanne jioni wameanza mazoezi rasmi kwenye uwanja wa Chuo cha Biblia katika mji wa Bigwa pembezoni ya Manispaa ya Morogoro.

Baada ya mazoezi meneja wa Yanga Hafidh Saleh amezungumza kuhusiana na maandalizi yao kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba Aprili 29, 2018.

“Tumeanza mazoezi Morogoro, kila kitu kipo sawa wachezaji ambao walikuwa majeruhi wamerudi kwenye kikosi nadhani maandalizi yataendelea vizuri kabla ya kuikabili Simba siku ya Jumapili.”

“Chirwa ana matatizo ya kifamilia, Tshishimbi alikuwa anaendele na matibabu lakini wapo njoani wanakuja Morogoro kuungana na sisi.”

“Tutakuwa hapa hadi Jumamosi tutarejea Dar kwa ajili ya mchezo wetu siku ya Jumapili.”

Mashabiki wa Yanga walijitokeza kwa wingi kuimarisha ulinzi kama ilivyokuwa kwa wenzao wa Simba ambao walifanya mazoezi Jumanne jioni uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here