Home Kitaifa Kinda wa Lipuli afichua ubora wake

Kinda wa Lipuli afichua ubora wake

10908
0
SHARE

Kiungo kinda wa Lipuli na timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ Shaban Ada amekuwa katika kiwango cha juu katika mechi za VPL ambazo ameichezea timu yake.

Ada ambaye ni zao la Serengeti Boys iliyoshiriki michuano ya AFCON kwa vijana chini ya miaka 17 iliyofanyika Gabon mwaka 2017, ameaminiwa na klabu yake na kupewa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Amesema ubora wake unatokana na bidii kujituma pamoja na nidhamu huku akiwa na njaa ya mafanikio ili kutimiza ndoto zake pamoja na kuisaidia familia yake.

“Kujituma tu, ukishajua unatoka kwenye familia yenye njaa ukikubali kufanya hovyo basi utaendelea kubaki kwenye shida kwa hiyo najitoa ili nisaidie familia yangu, ndugu zangu na mimi mwenyewe. Ukijituma kila kitu kinakuwa sawa, hakuna uchawi mazoezi jitihada, nidhamu ndiyo vitu vinavyonifanya nacheza.”

“Mimi pia natamani kucheza timu kubwa napenda siku moja nimiliki gari na nyumba yangu kwa hiyo nikicheza chini ya kiwango siwezi kufika huko. Lazima nipambane kwa ajili ya timu na hapo ndio nitaonekana na nitatimiza ndoto zangu.”

Ada amezaliwa Novemba 24, 2001 alikuwepo pia kwenye kikosi cha Ngorongoro Heroes kilichoitoa timu ya taifa ya vijana ya U20 ya DR Congo na kufuzu hatua ya pili kuelekea fainali za Afrika kwa vijana.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here