Home Kimataifa Bayern Munich kulipa kisasi cha 2013/2014 kwa Madrid hii leo?

Bayern Munich kulipa kisasi cha 2013/2014 kwa Madrid hii leo?

11948
0
SHARE

Kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes ameeleza wasiwasi wake kuhusu Cristiano Ronaldo wanapoikaribisha Madrid hii leo, lakini Heynckes pia amewaonya Real Madrid kuhusu madhara ya Roberto Lewandoski.

Jupp Heynckes  ana kumbukumbu nzuri na mbaya kwa Madrid, mnamo mwaka 1998 aliwapa kombe la Champions League lakini siku nane tu baada ya kuwapa kombe hilo alifungashiwa virago baada ya timu yao kumaliza katika nafasi ya 4 ya ligi.
Bayern Munich na Real Madrid hii leo wanakutana kwa mara ya 25 katika Champions League, hii ni rekodi kwani katika michuano hii hakuna timu ambazo zimekutana mara nyingi kama Bayern Munich na Real Madrid.

Hakuna mbabe kati ya hawa wawili kwani kila mmoja amwmfunga mwenzie mara 11, lakini kwa siku za karibuni Bayern Munich wanaonekana kuwa vibonde wa Madrid kwani wamepigwa mara 5 mfululizo.

Mchezo wa leo itakuwa mara ya tatu kwa wababe hawa kukutana katika nusu fainali ya Champions League tangu 2011/2012, katika nusu fainali mbili zilizopita Bayern Munich walifudhu ya 2011/2012 huku Madrid akifudhu ya 2013/2014.

Allianz Arena panaonekana mahala salama kqa Bayern Munich, katika michezo 16 iliyopita ya Bayern Munich katika uwanja huo wameshinda michezo 14, wakifunga mabao 48 na kuruhusu kufungwa mabao 10 tu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here