Home Kimataifa Salah, Firmino, Mane “cancer” mpya kwa mabeki Ulaya, waiua As Roma

Salah, Firmino, Mane “cancer” mpya kwa mabeki Ulaya, waiua As Roma

11179
0
SHARE

Hakika kama utaongelea utatu ambao kwa sasa duniani umeshindikana, baasi uko pale Liverpool. Roberto Firmino, Mohamed Salah na Sadio Mane wanaonekana cancer mpya kwa mabeki wa timu pinzani. 

Wanaonekana kufanya wanavyotaka, na kwa mara nyingine wameshuhudiwa wakiiteketeza bila huruma As Roma kwa kuitwanga mabao 5 kwa 2 katika nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Champions League.

Mo Salah alifunga mabao mawili ya kwanza na kumfanya kufikisha mabao 10, idadi ambayo ilimfanya kuwa mchezaji wa kwanza wa Liverpool kufunga idadi hiyo ya mabao katika msimu mmoja wa Champions League.

Salah pia amefikisha idadi ya mabao 43 akiwa na Liverpool msimu huu, na ni Ian Rush pekee katika msimu wa 1983/1984 ndiye ambaye amewahi kufunga idadi ya mabao mengi kuliko mabao ya Salah (47).

Lakini wakati watu wakiamini Salah leo anaweza kumaliza mpira akiweka rekodi ya mabao hayo 10 kwa Liverpool katika CL, Mbrazil Roberto Firmino naye alifunga mabao 2 na kuifikia rekodi ya mabao 10.

Mabao ya leo ya Firmino yanamfanya kuifikia rekodi ya ufungaji mabao 10 katika michezo michache zaidi, rekodi ambayo alikuwa nayo Adriano akifunga idadi hiyo ya mabao katika michezo 11.

Sadio Mane naye alifunga bao moja lililomfanya kufunga bao katika mechi 3 mfululizo za Liverpool nyumbani, lakini pia hii ilikuwa mara ya 8 kwa Firminho, Salah na Mane wote kufunga katika mchezo mmoja kwa Liverpool.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here