Home Kimataifa Liverpool vs As Roma, Klopp ataweza kuipeleka Liverpool fainali?

Liverpool vs As Roma, Klopp ataweza kuipeleka Liverpool fainali?

9308
0
SHARE

Baada ya mapumziko ya wiki mbili hatimaye Champions League imerejea tena. Hii leo kunapigwa mchezo wa kwanza wa nusu fainali ambapo Liverpool watakuwa Anfield kuikaribisha As Roma.

Hii ni nusu fainali ya kwanza kwa As Roma ndani ya miaka 27, ilikuwa msimu wa mwaka 1983/1984 ambapo Roma walikutana na Dundee United katika nusu fainali ya michuano hii na Roma akashinda na kwenda fainali.

Kuanzia mwezi March mwaka 2002 Liverpool na As Roma wamekutana mara 6(na hii ya leo), lakini katika mechi 5 zilizopita ambazo Liverpool wamekutana na As Roma wameshinda mechi 2, suluhu 2 na As Roma wakashinda mechi 1.

Liverpool wana rekodi mbovu katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Champions League, tangu 1984/1985 walipoifunga Panathinaikos , Liverpool hawajawahi kushinda mchezo wao wa kwanza wa nusu fainali ya michuano hiyo. Katika nusu fainali zao 7 kuanzia hapo walisuluhu 3 na kufungwa 4.

Pamoja na kutoshinda katika mechi ya kwanza ya nusu fainali lakini Liverpool wameshacheza nusu fainali 10, katika nusu fainali hizo 10 wamefanikiwa kupita na kucheza fainali mara saba.

Habari mbaya kwa Roma ni kwamba wakati wao wameshinda mchezo mmoja kati ya michezo 14 ya ugenini, Liverpool wenyewe wana rekodi ya kufunga mabao 33. Hii ni rekodi kwa klabu kutoka Uingereza kuwa na mabao mengi katika Champions League.

Edin Dzeko amehusika katika mabao 5 katika michezo 6 ya mwisho ya As Roma, na katika mechi 3 ambazo Dzeko ameichezea Roma dhidi ya Liverpool, kwa Liverpool Mo Salah akifunga kwenye mechi 4 za mwisho za Liverpool.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here