Home Kimataifa Daniele De Rossi, shujaaa wa As Roma asiyependa usharobaro wa wachezaji Instagram

Daniele De Rossi, shujaaa wa As Roma asiyependa usharobaro wa wachezaji Instagram

10986
0
SHARE

Muandishi mmoja nchini Italia aliulizwa kuhusu utemi wa De Rossi. Moja kati ya majibu ya muandishi huyu alisema De Rossi hapendi timu nyingine yoyote duniani zaidi ya As Roma na ndio sababu ukiwa timu nyingine ni rahisi kukufanyia ukorofi.

Daniele De Rossi ni mchezaji ambaye amekumbwa na matukio mengi mabaya yanayoletwa na utemi wake, mwaka 2006 alipewa kadi nyekundu katika hatua ya makundi ya kombe la dunia katika mchezo dhidi ya USA.

Baadaye De Rossi alimaliza kuitumikia adhabu yake katika michuano huku ikiendelea, na alikuwepo wakati Italia wanacheza fainali na kuisaidia kubeba ubingwa wa kombe la dunia mwaka 2006.

De Rossi amekuwa na matukio mengi sana ambayo pamoja na ubaya wake lakini yuko rohoni mwa mashabiki wa Roma, msimu huu ameshafanya tukio la kupiga viwiko mara mbili uwanjani, ameshaonekana akigombana na kocha wa timu ya taifa na pia bao zuri la kujifunga dhidi ya Barcelona.

Wakati Italia ikicheza mchezo wa pili wa kufudhu dhidi ya Sweden De Rossi dakika ya 58 aliambiwa apashe aingie, lakini bila matarajio ya wengi alimpayukia kocha na kumuambia wanatakiwa kushinda na sio kusuluhu na mtu wa kuwapa ushindi ni Lorenzo Insigne na sio yeye, baadae makocha waliona kweli na akaingia Isigne.

De Rossi ni mchezaji wa kizamani, anaongelea kuhusu dunia ya kisasa na mabadiliko yake haswa mitandao ya kijamii “dunia imebadilika sana, mimi natamani kumpiga mtu kofi wakati akiwa anajirekodi story katika Instagram, ni mambo ya ajabu sana”

Hii leo De Rossi atakuwepo uwanjani kuiongoza As Roma ambao watakuwa ugenini dhidi ya Liverpool nchini Uingereza, hii ni baada ya matokeo ambayo hayakutarajiwa ya As Roma kuwaondoa Barca katika robo fainali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here