Home Kitaifa CV ya kocha mpya wa Yanga

CV ya kocha mpya wa Yanga

17746
0
SHARE

Uongozi wa Yanga kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram umetangaza kuwa kocha atakaeifundisha timu hiyo amewasili nchini kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha wao mkuu George Lwandamina.

Kocha huyo anaefahamika kwa jina la Zahera Mwinyi ‘Mkongoman’ anatarajiwa kutambulishwa rasmi wakati wowote.

Zahera ambaye pia ana uraia wa Ufaransa amezaliwa miaka 46 iliyopita DR Congo na kufundisha vilabu kadhaa vya ndani na nje ya Afrika pamoja na timu ya taifa.

Julai 2010 aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa AFC Tubize ya Ubelgiji nafasi ambayo alidumu hadi Oktoba 2010.

Mwaka 2014 alirudi tena kuifundisha AFC Tubize akiwa kocha wa muda.

Agosti 2014 alitangazwa kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DR Congo na kuhudumu katika nafasi hiyo hadi Agosti 2017.

Amewahi pia kuifundisha klabu ya DC Motema Pembe ya DR Congo.

Lwandamina aliondoka Yanga akiwa bado hajamaliza kutumikia mkataba wake hadi mwisho na uongozi wa klabu hiyo haujatoa sababu yoyote ya kuondoka kwake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here