Home Kitaifa Bodi ya ligi imepokea malalamiko ya Yanga

Bodi ya ligi imepokea malalamiko ya Yanga

11410
0
SHARE

Bodi ya ligi kuu Tanzania bara imethibitisha kupokea malalamiko kutoka kwa klabu ya Yanga kuhusiana na mchezo wa Jumapili iliyopita kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Katika mchezo huo inaelezwa kuwa, mchezaji wa Mbey City alieoneshwa kadi nyekundu alirudi uwanjani kushangilia goli la kusawazisha la Mbeya City.

Tukio jingine ni wachezaji wa Mbeya City kucheza wakiwa 11 badala ya 10. Wakati mchezo ukiwa dakika za nyongeza kuna mchezaji aliumia akatolewa nje kwa ajili ya huduma ya kwanza.

Wakati akiwa nje benchi la ufundi la Mbeya City lilimfanyia mabadiliko lakini baada ya kufanyiwa huduma ya kwanza akarudi tena uwanjani na kufanya idadi ya wachezaji wa Mbeya City kuwa 11 sawa na Yanga.

“Tumepata malalamiko ya Yanga kwa hiyo tunapeleka kwenye kamati inayohusika kwa ajili ya maamuzi na kikanuni tunasubiri ripoti ya mwamuzi na kamishna ambazo tunakiwa tuzipate ndani ya saa 48”-aisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Michae Wambura alithibitisha jana jioni.

“Malalamiko yamekuja wakati mimi sipo ofisini, yamepokelewa na yamelipiwa lakini kilicholalamikiwa bado sijapata nafasi ya kusoma.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here