Home World Cup Morocco; Infantino apuuzwe anatumika na marekani

Morocco; Infantino apuuzwe anatumika na marekani

9919
0
SHARE

Kombe la dunia 2026 imefika patamu. Wakati wewe ukiwa huna hata mipango ya kesho, FIFA wao wanawaza kuhusu mwaka 2026. Ndio. Huenda ukiwauliza TFF mwaka 2020 mna mpango gani mpya hawajui. Enewei tuachane na hayo.

Tusafiri mpaka kunako Jiji la Rabat. Naam, katika nchi ya Morocco ambayo ina wingi wa watu takribani million 38. Wamorocco wanataka kombe la dunia lichezwe pale kwao mwaka 2026. Lakini wanapiga makelele kuwa mchawi wao mkubwa ni Giann Infanitno ambaye inaonekana nataka kuwadhulumu nafasi yao hiyo.

Dili lipo hivi.

FIFA wana tume yao ya uchunguzi. Wanakuja kama mashushu. Ni wadukuzi sana hao jamaa. Ni moja ya tume huru ya FIFA inayochukiwa zaidi na wadau wa soka maana inasemekana wao ndio wanakuwa na taarifa kamili. Ripoti yao ni muhimu zaidi. Wengine wana washutumu kuwa ndio wanaongoza kwa ulaji wa rushwa. Tume hii imeshaanza kampeni zao kwa mataifa yaliyoipleka zabuni.

Walianzia  Jiji la Mexico, kasha wakaibukia Atlanta, Toronto na New York. Safari hii ya sikua 4 ilifanyika katika viunga vya majiji haya kwa kuangalia vifaa vya mazoezi, viwanja, kempu za mapokezi na malazi,  maeneo ya mashabiki kuvinjari, usalama, Viwanja vya kuchezea, mara ya mwisho walizuru katika kiwanja cha Marcedes Benz Arena cha mjini Atlanta.

Safari ya Morocco

Morocco wanaongea lugha zaidi ya mbili Kiarabu, Berber, kiarabu cha Berber Hassaniya. Morocco ina maeneo mengi ya utalii nay a kuvutia.

Tume hii ilifikia miji kama Marrakesh ambao unasemekana kuwa unavutia zaidi kwa utalii hasa kutokana na mji huu kuwa na majengo ya zamani, miji mingine ni Tangiers, Agadir, na Casablanca mji huu unajulikana sana kwa kuwa na msikiti maarufu ujulikanao kama Msikiti Hassan II uliotengenezwa na wajenzi 10,000.

Shida imeanzia wapi?

Taarifa kutoka Morocco zinasema kuwa, hawa wachunguzi walipokwenda huko Amerika kaskazini walifanya kazi yao kwa upendeleo mkubwa. Walionekana kuwa walikuwa na moyo wa kufanya kazi hiyo. Wadau wa soka Morocco wanadai kuwa Infantino amepanga njama za kuwaondolea Morocco vigezo kwa kuwakwamisha baadhi ya taratibu za kufuatwa bila sababu za msingi.

Infantino nae
Inasemekana baada ya kuipitia Zabuni ya Morocco aliandika barua kwa FIFA akielezea kuwa haoni umuhimu wa zabuni ya Morocco hivyo aliwaomba washiriki wote wasifanye chochote na zabuni hiyo. Pia aliomba shirikisho la soka barani afrika likae kimya kwanza kabla hawajaungana pamoja kuunga mkono zabuni ya Morocco.

istoshe kwenye mkutano mkuu wa Shirikisho la soka barani afrika aliwanyima Morocco nafasi nafasi ya kuwakilisha zabuni yao, lakini mbaya zaidi aliruhusu mwakilishi kutoka marekani kufanya hivyo kwenye mkutano wa shirkisho la soka la kusini mwa Afrika COSAFA.

uwanja huu unaitwa Grande Stade De Cassablanca unabeba watu 93,000

Infantino Ni nani

Jina Kamili Giovanni Vincenzo Infantino
Kuz Mahali Brig, Switzerland
kuzaliwa 23/03/1970 (48)
Elimu Chuo kikuu cha Fribourg
Cheo Raisi wa FIFA
Cheo hapo awali Katibu mkuu wa UEFA
Mhuasiano Ameoa

Leena Al Ashqar (mlebanon)

Mshabiki wa Inter Milan

Infantino na Raisi wa Afrika.

Mwezi wa pili mwaka huu Infantino alizuru Cassablanca katika mkutano wa maendeleo ya soka la Afrika. Akasema hivi

“mnapaswa kuhakikisha kuwa zoezi hili linakwenda sawa na kwa aaraka zaidi”

Maneno haya ni kama yalijaa unafiki kwani alijua wazi ni mara ngapi amekuwa kikwazo kwa Morocco kuwakilisha zabuni yao. Mara baada ya kuongea, Rais wa CAF Ahmad Ahmad nae alisimama akanena

“ tunaishi sehemu yenye uhuru, mpo huru kufanya uamuzi wowote”

Ni kama alitupa vijembe kwa Infantino kwani aliongeza na kusema “nina nafasi kubwa kama kiongozi, waliopo nyuma yangu wananiunga mkono kila nalofanya, ila ni jukumu lenu kuamua”

Maneno haya aliwaambia wana Morocco akimaanisha kuwa yupo tayari kuunga mkono juhudi zao.

Moroco wanasemaje?

Taarifa za chombo kimoja cha kuaminika cha Moroco zimefufua kaburi na kudai kuwa Infantino anapanga njma za kuipa nafasi kubwa Marekani kushinda zabuni hiyo kwani Marekani ilimsaidia Infantino kuwa rais wa FIFA.

Hili linaweza likaibua mengine. Huenda lilatea hali mbaya na kuchafua hewa kwa infantino kama itagundulika ni kweli.

Taarifa za kudusuadusua zinasema aliyekuwa mwenyekiti wa shirkisho la soka la marekani mwaka 2016 bwana Sunil Gulati ndiye aliyempigia Infantino chapuo kubwa.

Baadhi ya vyombo vya Marekani kama The New Uork Times vilikiri kuwa Infantino alisaidiwa na marekani kumpiku Sheikh Salman bin Ibrahim al-Khali kutoka Bahrain.

Mbaya zaidi mtandao wa Bloomberg umedai kuwa taarifa za chini kwa chini zinasema kuwa Marekani imeiahidi FIFA mamilioni ya dola kama itapata nafasi hiyo. Je hii ni rushwa? Je damu ya Blatter bado inanuka?

Shrikisho la soka Morocco lanena?

Sisi tuepokea taarifa za kupeleka zabuni ikiwa zimesalia siku mbili kabla ya siku ya mwisho ya maombi. Kinachotusikitisha ni kwamba wameweka vijisababu ambazo kwenye vigezo vya mwandalzii wa mashindano havipo katika orodha ya vipengele vya FIFA , kwa mfano wamesema ukubwa wa viwanja vya ndege, wanadai eti ni vikubwa na vya gharama sana.

Mataifa mengine yalalama.

Norway kupitia mtandao mmoja wamesema kuwa, ukiangalia asili ya hawa wanajiita wachunguzi wa FIFA wengi wao ni watu wa karibu mno na Infantino. Watu wakisikia wachunguzi wanahisi ni watu ambao hawana ubaguzi, au ni watu waliochaguliwa kwa haki na usawa, lakini wengi wao wao wametumwa na watu fualni kwa jili ya matakwa yao.  Baadhi ya wachunguzi wa tume hiyo ambao wanatokea wamedai kuwa katika kufanya kwao kazi hakuna usawa kabisa na wakati Fulani wamekuwa wakitenga au kuupuza nchi za Afrika.

 

Maoni yangu?

Nimekagua baadhi ya ripoti za hao wakaguzi kutoka huko ulaya. Nimegundua kulikuwa na uanafiki mkubwa sana. Kwanza nimeona baadhi ya komenti zao kuhusu Morocco. Wanalalamika kuhusu mapokezi, mara wanasema hakuna ukarimu morocco, Mara hakuna viti vya VIP kwenye viwanja vyao nimeshanagaa sana. Kwani hayo mambo si yanarekebishika? Yaani leo hii unapima ukarimu wa watu kwa mtazamo wa watu kumi waliokuja siku 4?

Moulay Hafid Elalamy ni raisi wa soka wa Morocco, aliwajibu tu kirahisi, masuala ya viwanja ni mambo madogo kwa taifa hilo, hivyo ni vitu vinarekebishika. Tena wakitaka waje wawape tenda za kutengeneza viwanja wanavyotaka. Kuna mambo ya kutilia mkazo, kama hali ya hewa, usalama, miundo mbinu mingine kama barabara viwanja, usafiri n.k na sio  viti vya VIP kwa baadhi ya viwanja ambavyo Morocco wamesema wapo mbioni kuvirekebisha.

Najua Marekani ndio waliomtoa Blatter na Infantino anataka kulipa fadhila. Infantino ana deni kubwa sana kwa Wamarekani. Tatizo anakosea maana anaonekana waziwazi yupo tayari kukwamisha zabuni yeyote iatakayokuja mbele zake kuhakikisha kuwa Marekani wanaanda mwaka 2026.

 

Wachunguzi wamechukulia zabuni ya Morocco juu juu bila kujali mambo mengine ni mipango endelevu,

makala hii imeandaliwa na Priva Abiud (0763370020)

unaweza kunifollow Instagram kwa jina la Privaldinho na usisahau kupita Youtube kwenye channel ya dauda Tv kupata taarifa mbalimbali na usiache kusubscribe channel hiyo

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here