Home Kimataifa Mo Salah alistahili tuzo mbele ya De Bruyne, na atabeba nyingine

Mo Salah alistahili tuzo mbele ya De Bruyne, na atabeba nyingine

10132
0
SHARE

De Bruyne alistahili kupata tuzo ya mwanasoka bora nchini Uingereza, lakini wengine wanasema Salah amestahili. Mvutano huu umekuwa mkubwa sana hasa kutokana na uwezo wa hawa wawili.

Lakini je kwanini Salah ameshinda tuzo hii? Nilikuwa nasoma na kupitia maoni ya mashabiki wa soka mitandanaoni kuhusu tuzo hizi na mvutano umekuwa mkubwa sana, kila mtu akija na sababu zake, ikanibidi kufanya utafiti wa kina juu ya tuzo ya Salah.

Kwanza hii ni kati ya tuzo ngumu sana kumchagua mmoja kati ya Salah na De Bruyne, wote wanaonekana kuwa na msimu mzuri japo De Bruyne anabeba kombe la EPL huku Salah akibaki nafasi ya 3, pengine wapo walioona hii ni sababu ya kumpa tuzo KDB.

Lakini Mo Salah ana jambo kubwa zaidi kuliko EPL, Salah anakaribia kubeba Champions League(sahau alivyoibeba Misri kuelekea Urusi) , na hata kama Liverpool wasipobeba kombe hili lakini ni wazi kwamba Mo Salah amechangia kwa kiasi kikubwa kuifanya Liverpool kuwa timu pekee toka EPL iliyobaki Champions League.

Kwa Man City nako De Bruyne anatajwa kama moja kati ya watu waliosaidia kuipa City ubingwa lakini Je ni kweli Man City walitegemea mchango wa De Bruyne kubeba kombe? Bila yeye wasingebeba kombe? Jibu ni hapana lakini Liverpool wangemkosa Salah pengine hata nafasi ya 3 EPL wasingekuwepo.

Achana na De Bruyne ambaye alikuwa na ukame wa mabao msimu huu tangu January(mechi 13), lakini mabao 41 ya Salah kwa Liverpool yanaonesha kwa namna gani Mmisri huyu aliibeba Liva mabegani mwake, katika mechi 17 za Liverpool mwaka 2018 ni mechi 3 hajafunga na akifunga jumla ga mabao 18.

Timing ya tuzo hizi imemsaidia sana Salah kwani tuzo hii inatolewa wakati ambao ligi bado zinaendelea, uwepo wa Liverpool Champions League umembeba Salah, lakini vipi kuhusu tuzo ya waandishi wa habari ambayo hufanyika wakati ligi zikiwa zimeshaisha?

Swali hilo hapo juu ni muhimu kujiuliza, na je kama Liverpool watakosa Champions League Salah atamshinda tena De Bruyne katika tuzo hizo? Swali hili inatubidi kurudi hadi mwaka 1999 tuone nini kilitokea katika situation ya namna hii.

Kama utakumbuka huu ndio mwaka ambao David Ginola raia wa Ufaransa alikuwa katika kiwango cha hali ya juu wakati huu ambao alikuwa akiichezea Tottenham Hotspur na msimu huu ndio United walibeba FA, Champions League na Epl.

Nini kilitokea? Pamoja na United kubeba makombe yote matatu lakini David Ginola alibeba tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu nchini Uingereza na tuzo ya mchezaji bora wa waandishi wa habari za michezo Uingereza.

Jambo hili lililotokea kwa Ginola linaonekana ndilo ambalo linawatokea David Silva, Leroy Sane, Kelvin De Bruyne na Raheem Sterling, hata kama Liverpool hawatachukua kombe lolote lakini uwezo wa Salah ni mkubwa na anastahili kubeba tuzo nyingine.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here