Home Kitaifa Ni Mtibwa au Singida kimataifa 2019

Ni Mtibwa au Singida kimataifa 2019

3394
0
SHARE

Singida United kwa mara ya kwanza imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya kombe la TFF baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa nusu fainali uliochezwa uwanja wa Namfua Singida.

Mchezo huo uliochezwa kwa dakika 120 ulimalizika kwa sare ya 1-1 baada ya dakika 90. JKT Tanzania ndio walikuwa wakwanza kupata goli lililofungwa na Hassan Matelema dakika ya 38 ambalo lilidumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Singida United walifanikiwa kusawazisha mfungaji wa goli akiwa ni Tafadzwa Kutinyu ambapo hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zilikuwa sare kwa kufungana 1-1.

Dakika 30 zikatumika ili kumpata mshindi kwa mujibu wa kanuni, dakika ya 97 Kutinyu kwa mara nyingine akaifungia Singida bao bao la pili na la ushindi kwa upande wa Singida United.

Kwa matokeo hayo Singida United inatarajiwa kupambana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa fainali utakaochezwa Juni 2, 2018 mkoani Arusha kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo mshindi ataiwakilisha Tanzania bara kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here