Home Kitaifa Yanga imepoteza pointi mbili Mbeya

Yanga imepoteza pointi mbili Mbeya

9320
0
SHARE

Mbeya City ikiwa na wachezaji 10 uwanjani imeilazimisha Yanga sare ya kufungana 1-1 katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa uwanja wa Sokoine Mbeya.

Mbeya City ililazimika kucheza pungufu kwa dakika zaidi ya 25 baada ya beki wake Ramadhani Malima kutolewa nje kwa kadi ya nyekundu baada ya kuoneshwa kadi mbili za njano.

Kiungo wa Yanga Raphael Daudi ambaye ametokea Mbeya City alianza kuifungia goli Yanga dakika ya 56 lakini Idd Suleiman aliyetokea benchi akaisawazishia Mbeya City dakika ya 90+1.

Yanga imepoteza pointi mbili ambazo zingeifanya iisogelee Simba ambayo jana ilitoka sare ya kufungana 1-1 na Lipuli kwenye uwanja wa Samora, Iringa.

Kwa hiyo gape la pointi kati ya Simba na Yanga limeendelea kubaki vilevile, Simba ina pointi 59 katika nafasi ya kwanza baada ya mechi 25 huku Yanga ikiwa nafasi ya pili kwa pointi zake 48 ikiwa imecheza mechi 22.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here