Home Kitaifa Simba macho yote kwa Yanga

Simba macho yote kwa Yanga

11578
0
SHARE

Baada ya kubanwa na Lipuli na kujikuta ikiambulia pointi moja mkoani Iringa, sasa mipango ya Simba ni kushinda mechi yao ijayo dhidi ya Yanga ili kuendeleza gap la pointi dhidi ya watani wao wa jadi katika mbio za ubingwa VPL msimu huu.

Mjumbe wa kamati ya utendaji Simba Said Tully alizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo wao dhidi ya Lipuli na kusema, maandalizi yanaanza kuelekea mchezo dhidi ya watani zao Yanga.

“Tumepokea kama moja ya matokeo ya mpira lakini nia yetu haikuwa kupata pointi moja bado safari inaendelea kwa sababu kuna mechi zinaendelea kwa namna tulivyojipanga tunaamini kwamba tuna nafasi ya kuwa mabingwa.”

“Sare hii isiwakatishe tamaa wana Simba, wajue kwamba timu yao inafanya vizuri na inapambana kuhakikisha inafikia malengo.”

“Wanaotufuata sisi hawana uhakika wa kushinda mechi zote, tunaamini Aprili 29 tutazidi kuongeza gape dhidi ya wapinzani wetu kwa sababu wao ndiyo timu inayotufuata kwa karibu.”

Mechi kati ya Simba na Yanga inatarajia kuchezwa Aprili 29, 2018 ikiwa ni mechi ya ya pili Simba ikiwa mwenyeji wa mchezo huo, mchezo wa watani wa jadi katika raundi ya kwanza ulimalizika kwa sare ya 1-1.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here