Home Kitaifa Mkuu wa Wilaya amtabiria makubwa striker Lipuli

Mkuu wa Wilaya amtabiria makubwa striker Lipuli

9969
0
SHARE

Mshambuliaji wa Lipuli FC Adam Salamba Jumamosi ya Aprili 21, 2018 aliifungia timu yake bao ilipocheza dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Samora Iringa mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana 1-1.

Salamba alicheza kwa kiwango cha juu kwa kuisumbua vilivyo safu ya ulinzi ya Simba muda wote wa dakika 90 za mchezo.

Baada ya mechi Mkuu wa Wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela ambaye aliushuhudia mchezo huo alisema, ameutiwa na kiwango kilihooneshwa na Salamba na huenda akafika mbali kama ataendelea kuwa katika kiwango hicho.

“Nimefurahishwa sana na Adam Salamba ni mchezaji mzuri sana, nadhani akiendelea hivyo atafika mbali sana.”

“Mchezo aliocheza Salamba ametikisa beki yote ya Simba mpaka walikuwa wanachanganyikiwa.”

Kasesela pia alisema kwa kiwango kilichooneshwa na Lipuli, walistahili kushinda mechi hiyo lakini walishindwa kutumia nafasi nyingi kufunga magoli.

“Walicheza mpira mzuri sana na ukiangalia walikosa nafasi nyingi sana, kiuhalisia walitakiwa kushinda lakini ndio matokeo ya uwanjani.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here