Home Kitaifa Mbeya City yaigomea Yanga

Mbeya City yaigomea Yanga

11015
0
SHARE

Uongozi wa Mbeya City kupitia afisa habari klabu hiyo umesema kama klabu haitakubali kufungwa na Yanga kwenye uwanja katika mchezo wa ligi kuu unaotarajiwa kuchezwa uwanja wa Sokoine-Mbeya.

Afisa habari wa Mbeya City Shah Mjanja amesema wakati Mbeya City inafungwa na Yanga 5-0 Dar iliwakosa nyota wake wengi muhimu ambao walikuwa na majeraha.

“Wakati tunafungwa 5-0 na Yanga ilichangiwa na kuwa na wachezaji wengi wenye majeraha, wachezaji karibu watano walikuwa wanamajeraha. Timu inacheza kwa mfumo sasa mfumo ukiharibiki, mfumo ukiharibika timu inapoteza nguvu ya ushindani.”

“Wiki hii tupo vizuri tangu mechi dhidi ya Simba wachezaji wana afya nzuri na morali kubwa kwa hiyo nina imani kuwa mchezo huu utakuwa mgumu kwa sababu nilizozitaja.”

“Kama klabu hatutakubali kufungwa tumejiandaa kwa ajili ya ushindi dhidi ya Yanga.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here